.Huawei kufanya mfumo wa mawasiliano wa Airtel 2G na 3G kuwa wa kisasa zaidi na hata kuzidi kupanuka
.Ushirikiano huu wa kibiashara utaiwezesha Airtel Afrika kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwa wa gharama nafuu zaidi na mawasiliano yenye viwango vya kimataifa
Bharti Airtel,kampuni ya mawasiliano inayoongoza ulimwenguni,ikiwa inaendesha shughuli zake katika nchi 19 barani Afrika na Asia, leo imetangaza kuingia mkataba wa makubaliano na Huawei, kampuni mahiri katika mfumo wa mawasiliano katika zama mpya, ili kuweza kuimarisha, kupanua na hata kufanya miundombinu ya mfumo wa mawasiliano wa Airtel 2G na 3G kuwa wa kisasa zaidi barani Afrika.
Katika makubaliano haya, Huawei itakuwa na majukumu ya kuunda, kupanga, kupanua na hata kufanya mtandao wa Bharti Airtel kuwa ya kisasa zaidi, hii ikiwa ni pamoja na kusimamia uendeshaji na matengenezo ya mfumo wa mawasiliano.
Muundo huu wa usimamiaji na uendeshaji wa huduma za kibiashara kiubunifu, ambao umekuwa ukitumiwa naAirtel hiko India kwa takribani miaka nane iliyopita, unatarajia kuleta hamasa na mwamko wa kipekee katika ubora wa huduma kwa wateja, hususani kuhusiana na usikivu thabiti pamoja na mawasiliano kuweza kuwafikia hata wale walio maenneo ambayo hayakudhaniwa kufikiwa hapo kabla.
Aidha, makubaliano haya yataiwezesha Airtel Afrika kuweza kutanua na kusheheneza kwa haraka zaidi huduma zake za mawasilani ya simu na intanet barani kote.
No comments:
Post a Comment