Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nguruka,mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo aliwaeleza wananchi kutoa ushirikiano kwa wajenzi wa barabara ya lami ya Malagalasi-Nguruka yenye urefu wa Km 48, sambamba na ujenzi wa daraja la kihistoria la Malagalasi lenye urefu wa mita 275

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila (kulia),akipongezwa na Diwani wa Kata ya Itebula (NCCR-Mageuzi), Shukuru Chiza baada ya kuhutubia mkutano wa kuwashukuru wananchi waliompigia kura katika Kata hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Jimbo, Venance Mwaka. Mkutano huo ulifanyika katika Kata hiyo mwishoni mwa wiki.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja wa Wakala wa Barabara wa Serikali (TANROADS), Mkoa wa Kigoma,Haruna Senkuku (wa pili kushoto) pamoja na Katibu wa Mkoa wa Kigoma, Sekulu wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa daraja la kihistoria la Malagalasi lililopo katika Jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu, Joseph Simbakalia (katikati) walipokuwa wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Barabara wa Serikali (TANROADS), Mkoa wa Kigoma,Haruna Senkuku kuhusu ujenzi wa Barabara ya kwanza ya lami ya Kidahwe-Uvinza yenye urefu wa Km 76 inayojengwa Jimbo la Kigoma Kusini,mkoani Kigoma. Viongozi hao wawili walitembelea mradi huo mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia (aliyevaa suti nyeusi) pamoja na vingozi wengine wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila wakiangalia eneo patakapojengwa daraja jipya la Mto Malagalasi, walipotembelea eneo hilo hivi karibuni.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akimuuliza jambo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (katikati aliyevaa tai) walipokuwa wakikagua ujenzi wa Barabara ya kwanza ya lami ya Kidahwe-Uvinza yenye urefu wa Km 76 inayojengwa Jimbo la Kigoma Kusini,mkoani Kigoma. Viongozi hao wawili walitembelea mradi huo mwishoni mwa wiki.Picha na Richard Mwaikenda.
No comments:
Post a Comment