HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 7, 2011

VODACOM MISS ARUSHA CITY CENTER KUFANYIKA MEI 13.

Mashindano ya ulimbwende ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini, Vodacom Miss Arusha City Center 2011 yanatarajiwa kufanyika mei 13 katika ukumbi wa Triple A, Arusha.

Akizungumza na blog hili, mraribu wa shindano hilo Bi. Sophia Urio alisema kuwa kwa sasa wamejiandaa vyema tayari kwa ajili ya kufanya umashindano hayo rasmi yatafanyika Mei 13 katika Ukumbi wa Triple A jijini humo.

Mpaka sasa wamehakamilisha wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo wenye mvuto na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu wanatokea mkoani Arusha.

"Tunamshukuru Mungu kwa maandalizi ambayo tumeshayafanya mpaka sasa, tunachosubiri kwa sasa ni uzinduzi wa mashindano hayo ili tuweze kuendelea na kila kitu," alisema Bi. Sophia Urio.

Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi.

Wadhamini katika shindano hilo ni Vodacom, Startimes, Stone, Shuphaa Quality boutique, Janeths Beaty Parlour pamoja na Africasana Pub iliyopo Holili, Moshi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad