HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 7, 2011

TIGO YASAIDIA KUWEZESHA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM.

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Terezya Huvisa katika zoezi la kufanya usafi kuhakikisha jiji linakuwa safi lililofanyika leo asubuhi jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Terezya Huvisa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Jackson Mmbando (kushoto) akifafanua juu ya zoezi hilo ambalo alisema litakuwa linafanyika kila jumamosi ya kwanza ya mwezi lengo lake kuu ni kuweka jiji safi.Askari wa JKT nao hawakuwa nyuma.Mgambo wa jiji la Dar es Salaam nao wakiwajibika.Wananchi wakiwajibika kuweka jiji safi.Watu mbali mbali waliojitokeza katika zoezi hilo.Wanafunzi na watu mbali mbali walijotokeza.

Katika mkakati wa kuhakikisha mazingira ya jiji la Dar es Salaam yanakuwa katika hali ya usafi wakati wote, Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imetoa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dar es Salaam, vyenye dhamani ya shilingi milioni nne.

Vifaa hivyo ambavyo vimekabidhiwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Terezya Huvisa ni pamoja na mafyekeo, Reki, Koleo na mifuko ya kuzolea taka.

Katika makabidhiano hayo ambayo yaliendana na zoezi la kufanya usafi katika sehemu mbali mbali ya jiji la Dae es Salaam ambapo zoezi hilo lilifanywa na askari wa JKT, askari wa jiji la Dar es Salaam, wanafunzi wa shule za sekondari mbali mbali za Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Tigo.

Nae ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Jackson Mmbando alisema kuwa mbali na kuboresha huduma kwa wateja wake, kampuni hiyo inamambo mengi ya kuwafanyia watanzania.

Aliongeza kuwa Tigo Inayofuraa kuona watanzania wanaishi katika mazingira mazuri ili waweze kupata afya njema kwa ajili ya kuwajibika katika shughuli mbali mbali.

Safisha jiji programu ya endelevu ambayo ilitangazwa na ofisi ya makamu wa Rais kuwa kila jumamosi ya kwanza ya mwezi kuanzia saa 1.00 asubuhi mpaka saa 4.00 asubuhi ni siku ya kufanya usafi katika miji mbali mbali hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad