HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 11, 2011

SEND OFF YA DA' CLARA MOKILI YAFANA SANA

Bi. Haruzi mtarajiwa,Clara Mokili akiwa na Matron wake katika sherehe ya send off yake iliyofanyika katika ukumbi wa YMCA,Moshi mkoani Kilimanjaro mwinshoni mwa wiki iliyopita.
Clara akimimina Shampeini kwenye glass kwa staili yake.
Bi. Harusi mtarajia na Matron wakigonganisha glass.
Kekizz ikikatwa kwa ustadi mkubwa.
Wapendanao haooooo,hapo ni Bw. Nazareth Ndekia na Bi. Clara Mokili wakiwa na nyuso za furaha katika sherehe hiyo ya Send Off,ambapo sherehe ya ndoa itafanyika mwisho wa wiki hii.sasa kama hukupewa kadi ya mwaliko basi jua imekula kwako,mwenzenu nishapewa yangu.
Bw. Harusi mtarajiwa,Nazareth Ndekia akipungia wageni waalikwa mara alipokuwa akitambulishwa katika send off hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa YMCA uliopo Moshi mkoani Kilimanjaro.
Wakielekea hai tebo.
alipopatikana baada ya kusakwa ukumbi mzima.na hapo Matron anamuuliza Bi. Harusi kama huyu jamaa ndio yeye au la maana walizunguka sana humo ukumbini.nae Bi. Harusi anajibu kwamba "Mtu chake mamaa.... yaani hapa hata sijachakachua" haha ahha ah.... kiukweli ilipendeza sana.
Baba wa Bi. Harusi,Mzee Mokili akikata kipande cha ndafu kucheki kama chumvi imekolea kabla ya kumlisha mwanae.
Baba na Mama wa Bi. Harusi mtarajiwa wakiwa wamebebwa juu juu ukumbini hapo iliwa ni sehemu ya pongezi toka kwa ndugu wengine.
Nazareth Ndekia na Mie niliekuwa nimejitoa kimasomaso siku hiyo kula dili na dobi wa mtaani kwetu ili anidundishie hii pamba ya mteja wake walau kwa siku 2 na nikafanikiwa hilo na mambo yakawa kama inavyoonekana picha hii.
Hii ndio familia ya Mzee Mokili yenye watoto sita kama waonekanavyo pichani hapo.
Magoma yamekoleaaa......

3 comments:

  1. ya kwako sijui lini? hujisikii hata uchungu unapopiga hizi picha za wenzio? shauri yako na muda si mrefu sheria ya kukataza michango ya harusi itapitishwa itakula kwako...

    ReplyDelete
  2. Sawa kaka,nami nitatangaza nia siku si nyingi ila ndio niko kwenye mchakato wa kumtafuta mwenza.kama vp waweza nisaidia katika huo mchakato ili kabla Zoezi la kuchangisha michango ya harusi halijanipata.Hahah Hahah Hahah ......

    ReplyDelete
  3. Duh! hiyo picha ya familia ya mzee Mokili imetoka bomba sanaaaaaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad