HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 3, 2011

SAFARI LAGER YAZINDUA MASHINDANO YA POOL KWA VYUO VYA ELIMU YA JUU

Afisa Mahusiano wa TBL,Dorice Malulu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano ya mchezo wa Pool kwa vyuo vya elimu ya juu nchini.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukondo.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo wametangaza rasmi kuanza kwa mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kwa mwaka 2011.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Meneja wa bia ya Safari,Oscar Shelukindo alisema TBL kupitia bia ya safari kwa mwaka huu imeongeza sehemu ya udhamini wake katika mchezo huo ambapo imeweza kuongeza mikoa ya vyuo vikuu kutoka mmoja wa mwaka jana hadi kufikia mikoa minane.

Bwana Shelukindo alisema mashindano hayo kwa mwaka jana yalishirikisha mkoa wa Dar es salaam pekee ambapo chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kilifanikiwa kuwa mabingwa wa kwanza kwa mwaka jana.

Alisema kwa mwaka huu mashindano hayo yatahusisha mikoa ya Dar es salaam, Morogoro,Dodoma,Mwanza,Iringa,Mbeya, Kilimanjaro na Arusha ambapo fainali za kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika mkoani Dodoma mwanzoni mwa mwezi june.

Mashindano katika ngazi za mikoa tayari maandalizi yake yamekamilika ambapo yataanza na mikoa ya Morogoro na Dodoma na mkoani Morogoro fainali ni jumamosi ya May 07,2011 zitafanyika katika ukumbi wa DDC na mkoani Dodoma ni jumapili May 08,2011 katika ukumbi wa Royal.

Kuhusu zawadi alisema mwaka huu katika ngazi ya mkoa na kitaifa jumla ya shilingi milioni kumi na nane na laki sita (18,600,000.00) zitatolewa kwa ujumla ambapo alisema fedha hizo na zawadi nyingine nyingi zitafanikisha kusaidia wanavyuo kuweza kupata namna ya kuongeza ufanisi wa kimasomo lakini pia kuweza kupata changamoto ya kukutana miongoni mwa wanavyuo wa chuo kimoja na kingine.

Alisema zawadi za mikoa mchanganuo wake ni mshindi wa kwanza kupata shilingi laki tano(500,000.00) mshindi wa pili laki tatu (300,000.00) mshindi wa tatu laki mbili (200,000.00) na mshindi wa nne shilingi elfu hamsini (50,000.00) na mchezaji mmojammoja mshindi ni laki moja (100,000.00) na mshindi wa pili elfu hamsini (50,000.00).

Ngazi ya taifa ni shilingi milioni mbili (2,000,000.00) mshindi wa pili ni milioni na laki tano (1,500,000.00) mshindi wa tatu milioni na laki tatu (1,300,000.00) mshindi wa nne milioni moja (1,000,000.00) na washindi wa tano hadi wa nane watapata kifuta jasho cha shilingi laki tano (500,000.00) kila chuo. Ambapo upande wa mchezaji mmojammoja mshindi laki tatu (300,000), wapili laki mbili (200,000) mshindi wa tatu laki na nusu (150,000.00) na mshindi wa nne laki moja (100,000.00)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad