
Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Mh.Sophia Simba akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kliniki ya macho kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) iliyo chini ya Shirika linalojihusisha na kuwasaidia watu hao linalofahamika kwa jina la UNDER THE SAME SUN (UTSS) katika makao makuu yake hapa nchini yaliopo Mikochoni Jijini Dar.

Daktari wa Macho kutona nchini Marekani,Dkt. Rebecca Kammer akizungumza na Bw. Elisha Ngeleja ambeye ni mlemavu wa ngozi na mmoja kati ya wafanyakazi wa Shirika la UNDER THE SAME SUN kuhusu uwezo wake wa kuona wakati akiwa katika shughuli zake za kila siku.katikati ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mh.Sophia Simba akifuatilia mazungumzo hayo leo katika ofisi za Shirika hilo,jijini Dar.

Dkt. Rebecca Kammer akionyesha namba za kuweza kupima uwezo wa mtu kuona wakati wa uzinduzi wa kliniki ya matibabu ya macho kwa watu wenye ulemavu ngozi.

Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Mh.Sophia Simba amuuliza swali mtoto George uwezo wake wa kuona baada ya kuangaliwa macho yake na Dkt. Rebecca Kammer leo.

Baadhi ya Miwani itakayotolewa kwa watakaopimwa macho katika kliniki hiyo.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la UNDER THE SAME SUN hapa nchini,toka kulia ni Elisha,Omary,mdau,Mwamlima,Names na mwisho ni Gamalieli.

Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Mh.Sophia Simba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirika la UNDER THE SAME SUN,Peter Ash (tatu kulia) na viongozi wengine wa Shirika hilo leo mara baada ya kuzinduliwa kwa kliniki ya macho.
No comments:
Post a Comment