Hakuna siri kwamba Babu nimekwunywa maji ya bendera na kulamba masizi ya mwenge wa Manchester United, naipenda ajabu timu hii, unaweza kusema katimu ketu haka kamezaliwa na bahati mkononi lakini jana bwanaaaa, dah!
OK, tuseme hivi, nina wasiwasi sana kama Barcelona wanafundishwa na kocha wa dunia hii, maana jana muda wote wa fainali ile ya UEFA uso wangu nilikuwa nimeuficha chini ya kiti. Jamaa yangu Valencia kila wakati akimbutua madaluga bwana mdogo Messi, bahati nzuri jana refa alisahau kadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, la sivyo jana Valencia alikuwa ni mtu wa nyekundu. Jana maji yalikuwa ya shingo, wacha mchezo bwana.
Bwana mdogo Park, big up sana, japo tumefungwa lakini wewe ndio hasa kifuta machozi changu. Dogo jana kajitahidi sana kuharibu pasi za Barca, japo jamaa walipoweka ubao kwenye tv palee kitu kikawa kinasoma "COMPLETED PASSES: Barca 200, Man 100". Nikasema kazi ipo.
Anewei, unapofungwa na timu ya wanaume kama Barca, ndio nimesema wanaume, mechi ya jana ilikuwa ni mechi kati ya wanaume na wavulana, sasa unapofungwa na timu kama Barca unakaa kimya kwanza, usikimbile kuongea, kila mwenye swali atajijibu mwenyewe, maana jinsi masaa yanavyozidi kupita ndio ninavyozidi kugundua kwa nini jana tumepigwa 3-1, tena kwenye udongo wetu wenyewe.
Hata hivyo hili moja limeweka heshima, hata braza Fagasoni mwenyewe, mzee wa big G, anaelewa hilo, kwani hukuona alivyoshangilia? Baada ya pale hata Fagasoni mwenyewe akasema hata wakishinda hawa jamaa haina kwere, tumejaribu.
Ila tuzungumze yote katika mpira wa jana lakini mwisho wa yote turudi kwenye swali moja tu, "Barca wanacheza mpira wa kitabu kipi?" Swali hili muhimu sana, maana ushindi Barca mwaka huu umeziacha timu zote bab'kubwa zikibaki na sifa ya U-joka wa kibisa.
Hakuna asiyekumbuka aibu waliyovalishwa Real Madrid, tusahau hiyo, hii ya jana dah! Nacheki kwenye ubao naambiwa "BALL POSSESSION: Barca 70%, Man U 30%", nikabaki nang'ata kucha tu kwa hasira.
Ila leo nimeamka salama, nimeelewa kwa nini jana tumechezeshwa safa, Barca hawachezi mpira wa dunia hii. Ni wakati sasa wa timu zingine kuanza kusaka hicho kitabu wanachotumia Barca. Barca wameanza kunikera kwa ukijogoo wao, ni wakati wa timu flani, nadhani itakuwa Man U, mmmhmmhh, kuanza kujenga upinzani kimtindo, yale mambo ya kupigishwa safa jana sio kabisa.
Messi akikatiza kichakani mwa Man U.
Hakuna anayebisha kwamba mafanikio ya Barca ni matokeo ya uongozi safi wa kitimu wa kocha Pep Guardiola, kocha mtu wa watu, amefanikisha kuurithi vyema mtindo wa mpira wa Barca, mtindo wa pasi fupi na haraka, mtindo ambao hata yeye aliucheza alipokuwa mchezaji wa Barca.
Ni uongozi wake uliotumia, uongozi unaorihusu wachezaji kuongeza vitu vya kwao wenyewe, ni uongozi wa aina hii ndio unaoweza kukufanya ukajikuta unaishangilia Barca hata inapokufunga.
Big up Pep Guardiola
Anewei, Hongera Barca kwa ushindi wa UEFA Cup, Pedro, Messi, Rooney, nice goals people.
Bob Sankofa a.k.a Babukajda
Man U hamuwawezi Barca acheni utani, kwa hii ni mara ya 2 mfulululizo.Bora hata ingekuwa guners huwa wanajitahidi co nyinyi kazi kuongea tu.
ReplyDelete