HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 21, 2011

MASHINDANO YA POOL KWA VYUO VIKUU YA SAFARI LAGER

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager wanatangaza rasmi kuanza kwa mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kwa mwaka 2011.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo,Mratibu wa mashindano hayo Taifa Bw.Innocent Melleck (pichani) alisema mashindano hayo kwa sasa yameshafikia hatua ya fainali kwa mikoa minne ambapo tayari mikoa ya Dodoma bingwa ni St Johns University, Morogoro ni Sokoine University, Iringa Ni Ruaha University na Mbeya Bingwa ni Uyole Community Development Training Institute ambapo kwa sasa fainali itafanyika katika mkoa wa Kilimanjaro kwenye ukumbi wa Makanyaga uliopo Soweto ambapo patavikutanisha vyuo vya MUCOBS,Tumaini University,Stephano Moshi Memorial University College na St John University.

Siku ya jumapili fainali zitafanyika mkoani Arusha katika Ukumbi wa Songambele ambapo vyuo vitakavyopambana ni Arusha Institute of Accountancy na vingine vitatu.

Alisema baada ya kumaliza mikoa hiyo mashindano yataelekea Mwanza na Dar es salaam ambapo fainali za Dar zitafanyika June 28,29 katika ufukwe wa bahari ya Hindi Kwenye ukumbi wa Coco Beach.

Mabingwa wa mikoa yote watakutana katika fainali za kitaifa zitakazofanyika kwenye ukumbi wa Roya uliopo mkoani Dodoma kwenye tarehe 4,5 mwezi june ambapo zawadi zitakuwa ni shilingi milioni mbili (2,500,000.00) mshindi wa pili ni milioni na laki tano (1,500,000.00) mshindi wa tatu milioni na laki tatu (1,300,000.00) mshindi wa nne milioni moja (1,000,000.00) na washindi wa tano hadi wa nane watapata kifuta jasho cha shilingi laki tano (500,000.00) kila chuo.

Ambapo upande wa mchezaji mmojammoja mshindi laki tatu (300,000), wapili laki mbili (200,000) mshindi wa tatu laki na nusu (150,000.00) na mshindi wa nne laki moja (100,000.00)

Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba wakazi wa maeneo yote husika kujitokeza kwa wingi ili kuweza kushudia namna ambavyo mashindano hayo yalivyo na mawashawasha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad