HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 30, 2011

MASHINDANO KWA VYUO VYA ELIMU YA JUU MKOA WA DAR YAMALIZIKA

Mchezaji wa Pool kutoka Chuo cha CBE akimaliza mchezo kwa mbwembwe na kuifanya timu yake kuingia katika hatua ya fainali katika mashindano ya Safari Lager Pool kwa vyuo vya elimu ya juu,yaliyomalizika jana jioni katika ukumbi wa Coco Beach jijini Dar.hadi mwisho wa mashindano hayo timu ya Chuo cha IFM ndio walioibuka kidedea na kwa kuunyakua ubingwa huo na kujihakikishia kuingia moja kwa moja kwenye mashindano hayo kwa ngazi ya Taifa yatakayofanyikika mkoani Dodoma hivi karibuni na kukutanisha vyuo mbali mbali vilivyoshinda katika mikoa yake.
Mashindano yakiendelea.
Mchezaji kutoka Chuo cha DSJ akionyesha umahiri wake wa kusukuma mipira shimoni katika mashindano ya mchezo wa Pool kwa Vyuo vya Elimu ya Juu vya hapa jijini Dar,yaliyomalizika jana jioni katika ukumbi wa Coco Beach.
Umakini ukitawala mchezoni.
Watu wengi walijitokeza kuangalia mashindanyo hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad