HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 21, 2011

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA SHUGHULI ZA MAZISHI YA SHEIKH YAHYA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki (kulia) pamoja na baadhi ya viongozi, wakiwa kwenye shughuli ya mazishi wa aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, Sheikh Yahya, aliyefariki dunia jana jijini na anatarajia kuzikwa leo kwenye makaburi ya Tambaza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akijumuika na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu kuomba dua maalum kwa ajili ya marehemu Sheikh Yahya Husein, aliyefariki dunia jijini Dar es Salaam jana,dua hiyo ilifanyika nyumbani kwa marehemu Magomeni Mwembechai leo Mei 21. Maziko yatafanyika kwenye makaburi ya Tambaza leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mjane wa marehemu Sheikh Yahya, Kate Yahya, wakati alipofika nyumbani kwake Magomeni Mwembechai leo Mei 21 kuhudhuria shughuli za mazishi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiondoka nyumbani kwa marehemu Sheikh Yahya Husein, baada ya kuhudhuria shughuli za mazishi leo Mei 21, Magomeni Mwembechai Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi waliofundishwa na Marehemu Sheikh Yahya, wakiwa kwenye shughuli za mazishi nyumbani kwa marehemu Magomeni Mwembechai leo Mei 21. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad