HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 2, 2011

KUUWAWA KWA OSAMA BIN LADEN

Osama Bin Laden amefariki dunia, Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza hayo usiku wa kuamkia leo katika hotuba yake aliyoitoa kupitia luninga. Amesema kifo cha Bin Laden ni matokeo na juhudi za jeshi la Marekani likishirikiana na lile la Pakistan. Mauaji haya yamefanyika katika mji wa Abbottabad, Pakistani, katika nyumba aliyokuwa akiishi Bin Laden kwa kificho. Baada ya kurushiana risasi kwa muda na wanajeshi wa Marekani walifanikiwa kumuua Laden na kutoweka na mwili wake.

"Usiku huu natangaza kwamba jeshi la Marekani limefanya oparesheni iliyofanikisha kuuawa kwa Osama bin Laden" Alisema Rais Obama akiwa katika kasri lake, almaarufu kama White House, huko Washington.

"Haki imetendeka" Aliendelea kusema huku akiashiria kwamba shughuli ya kumuwinda Laden, kiongozi wa kigaidi, hatimae imefika tamati, shuguli ambayo imelitesa taifa la Marekani tangu mashambulizi ya Septemba 11 miaka kumi iliyopita.

Obama alisema kwamba taasisi za kiintelijensia zilipata kidokezo cha alipo Laden hapo mwezi Agasti mwaka jana, ni kidokezo hicho ndicho kilichofanikisha mashambulizi ya jana yaliyopelekea mauti kwa Laden. Rais Obama aliongeza kwamba alifikia uamuzi wa kuruhusu majeshi ya Marekani kufanya shambulizi la jana baada ya ushahidi wa kutosha juu ya uwepo wa Bin Laden katika eneo hilo kukamilika.

kwa habari zaidi iliyotafsiliwa kwa kimatumbi na mdau Bob Sankofa


2 comments:

  1. HII NI KWELI AU WAMAREKANI WANAVUMISHA KUUZA HABARI ISIJE KESHO UKASIKIA OSAMA HUYO HUYO KATOA TAPE MPYA ANAHOJIWA NA AL JAZEERA HALAFU UKASHANGAA!!!!!!!
    MIMI MPAPAKA SASA NIPO NJIA PANDA HADI NITAPO UONA MWILI WA OSAMA.
    KWANINI WANASHINDWA KUUONYESHA IKIWA TUKIO NI LA KWELI, KWANINI UFICHE FICHE HAPO BADO NNA MASHAKA.
    PILI MKUU VIPI MBONA TENA LINK YA BLOG YANGU HAPO KWAKO TENA HAIPO NADHANI
    NI BAADA YA MODIFICATION YA HIYO TEMPLATE SIJAIONA TENA.FANYA MPANGO
    TENA IWEKE http://allyshams.blogspot.com/ (24 SEVEN 365.
    NAIMANI UTAFANYA HIVYO MKUU NAKUAMINI.
    ASANTE

    ReplyDelete
  2. INNA LILLAHI WAINNA ILLAIHI RAJIUN,
    Kila mmoja wetu ataonja mauti kwa wakati wake,Osama ameshaonja na hataonja tena mengine na mwenye kujigamba kwamba kafanikiwa,nae atakwenda alikotangulia Osama ,Lakini ni kwa sababu gani kumdhalilisha kwa kumtupa baharini wakati anako alikozaliwa na watu wake?
    Kifo cha mja hakiashirii wema au ubaya wake,anaweza kufa kifo kibaya ikawa ndio wema kwake kwa nini amedhulumiwa na waliomfanyia kifo cha aina hiyo na anaweza kufa kifo cha kitandani hata aliekaribu nae asijue kama huyu mtu ameshakufa ,binaadamu tukasema amekufa kifo salama kumbe hakupata dakika za kalimatu tawhid.
    Afurahishwae kwa kifo cha mmoja wenu,watafurahishwa wengine kwa kifo chake.Maadamu ni muislam inafaa kumuombea dua kwa kusema.
    ALLA HUMMA KHFIR LAHUM WAARHAMHUM

    ReplyDelete

Post Bottom Ad