
Site Senta a.k.a Mjini Daslam na huu ni mtaa wa India jengo linaloonekana mbele ni hoteli ya Holiday Inn.

Posta mpya hapa pembeni mwa jengo la Benjamin Mkapa Tower,napo ni Town kabisa.

Hapa ni Uzuri pande za Tandale na hii ni moja tu ya sehemu zilizoharibika ila kuna sehemu nyingi tu zilizoharibika katika njia hii.

Buguruni Rozana hapa,yaani ndio hapasemeki kabisa kwa jinsi kulivyoharibika maana ukipita na gari yako kama iko chini chini unaweza kulia kwa namna itakavyokuwa ikipita kwa shida.

kiji bahari katika mtaa huu unaoelekea Peugeot House,yaani hadi inakuwa shida kupita kwa sisi watembea kwa miguu.

Mtaa wa Jamhuri jirani kabisha na jengo la Benjamin Mkapa.

Mtaa wa Likoma,Kariakoo imebidi waweke raundi abauti hii ya matairi ya magari ili kuepisha watu wasieze tumbukia kwenye shimo kubwa lililopo hapo katikati.
No comments:
Post a Comment