HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 5, 2011

Benki ya KCB Tanzania yatoa msaada kwa watoto yatima

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye na mfanyakazi wa benki hiyo tawi la Samora, Shose Kombe wakiwa wamewabeba watoto yatima wanaolelewa na Kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre cha Boko jijini wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula wenye thamani ya milioni 1.5/-.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye akimkabidhi mtoto Beatrice Phinius wa kituo cha watoto yatima Amani Orphanage Centre cha Boko moja ya misaada iliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa ajili ya watoto wa kituo hicho. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa kituo hicho Margaret Mwegalawa.
Meneja Masoko wa Benki ya KCB Tanzania Yusuf Shenyagwa akisaidiana na mfanyakazi mwenzake kushusha mchele uliotolewa na benki hiyo kwa kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.
Watoto yatima wa kituo cha Amani Orphanage Centre cha Boko jijini wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi msaada uliotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo wenye thamani ya milioni 1.5 kwa watoto 60 wanaolelewa kituoni hapo.


BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kufundishia kwa watoto wanaolelewa na kituo cha Watoto yatima cha Amani Orphanage Centre kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 1.5/- iliyofanyika kwenye kituo hicho kilichopo Boko nje kidogo ya jiji, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye amesema msaada huo umetokana na michango mbalimbali iliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo.

Akifafanua Christine amesema kwa kuwa wao ni taasisi ya kifedha wana wajibu wa kurudisha kiasi cha faida kinachopatikana kwa jamii na kwa kuanzia wafanyakazi wa benki hiyo walipendekeza msaada huo uanze kutolewa kwa yatima wanaolelewa na kituo cha Amani Orphanage Centre kutokana na uhitaji walionao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho Margaret Mwegalawa amesema licha ya benki hiyo kujitolea kukisaidia kituo chake kwa mara ya pili bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ubovu wa jengo na ukubwa wa jukumu la kuwalea watoto 60 wanaolelewa kituoni hapo.

Kwa upande wake Beatrice Phinius aliishukuru KCB Tanzania kwa kwa kuguswa na kuwapelekea msaada huo na kuomba taasisi zingine kujitokeza kuiga mfano huo.

Mwaka jana benki hiyo licha ya kutoa msaada wa` vifaa mbalimbali wenye thamani ya zaidi milioni 2/- kwa ajili ya takribani watoto 45, wa shule hiyo kile kinachopatikana, pia ilichukua jukumu la kuwalea watoto 11 wa kituo hicho kwa kuwanunulia vifaa muhimu vya shule.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad