
Alianza kufafanua kuwa, kwanza, tulijadili ni jinsi gani nchi zinazoendelea zilivyokuwa zikileta mabadiliko ya uchumi wa dunia, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya malengo ya milenia tuliyokubaliana.
Pili, tulijadili juu ya repoti ya bei ya vyakula inavyobadilika na kuongezeka katika dunia na athari ambazo tunatakiwa kuchukua ili kunusuru hali hiyo.Tulishauriana jinsi gani tuchukue hatua ya kuangalia uwezekano wa kubadilisha bei hizo hasa katika vile vyakula vya asili na athari zake hasa kwa zile nchi zenye watu wengi.
Tatu, tulijadili sera na matokeo ya utekelezaji wa ripoti ya maendeleo ya dunia katika mkingano, usalama , na maendeleo ya mwaka 2011. Mwaka huu ripoti hiyo itagawanywa gawanywa katika kuifanyia kazi na itaelekezwa kwenye Benki na washirika wanaounga mkono na kuchochea maendeleo na hali zilizo athiriwa na migongano na vita.
Mwisho ,tuliangalia wenyewe kwa kutaka kujua ni maendeleo gani tumeyafikia na niyapi yameimarisha taasisi za fedha za kundi la benki ya dunia.
Bw. Al Khalifa aliendelea kusema kuwa “mambo mengi yanayohusu mkutano huo yametolewa katika vipeperushi lakini ningependa kuyaelezea kwa kifupi sasa hivi:
Kwanza, kulikuwa na swali kwa nchi zinazoendelea.Maendeleo ya uchumi. Kwa ujumla, tunaona dalili za kukua kwa uchumi jumla, na nchi zinazoendelea ndio zimekuwa mbele zaidi katika kusaidia uchumi wa dunia kurudi katika hali yake, na vilevile nchi zinazoendelea ndio zimevuta uchumi huu kufikia hapa ulipo na kufanya uchumi kuendelea.
Kwa ujumla tunaona kuwa uchumi kwakweli unakua. Aidha nchi hizo zimesaidia kuiondoa dunia katika kipindi cha mpito, lakini tunatakiwa vilevile tujiangalie kwani kunadalili ambazo zinatakiwa kutupiwa macho.
Tunatambua kuwa kukuwa kwa mahitaji kwa haraka au kupanda kwa bei kwa haraka kwa baadhi ya sekta kunasababisha kuchochea bei kuwa juu na kutokuwa imara pia kuna sababisha mfumuko wa bei, hii ni hatari hasa kwa chakula na nishati, hivi vinaweka nchi zinazoendelea katika hatari hasa kwa nchi yenye watu wengi na ambao idadi yake inabadilikabadilika.
Mdororo huu wa uchumi kwa dunia na kupanda kwa bei ya vyakula na nishati ni vitu ambavyo vimechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma nchi zinazoendelea katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.
Katika makubaliano ya malengo ya maendeleo ya milenia tulikubali kuweka nguvu katika maendeleo ili ifikapo mwaka 2015 tuwe tumekwisha timiza malengo hasa katika maeneo yanayozungukwa na vitu vya hatari kama mabomba ya mafuta, maeneo ya hatari yenye historia ya kuwa na watu wengi ikiwa ni pamoja na wanawake na wasichana.
Pia tulijadili haja ya kuhakikisha kuwa bei ya vyakula inapungua na kuwa sio ya kubadilika badilika.Tulikaribisha utafiti uliofanywa na tunachukua hatua kutokana na maoni hayo.Tuna karibisha benki ya dunia kuchukua hatua katika maendeleo ya kilimo na kushawishi watafiti wanaoshughulikia kilimo cha uzalishaji ili kuja na suluhisho ambalo linaweza likaimarisha kilimo.
Hii inawahusu pia wafanya biashara wa kimataifa katika kilimo, kuimarisha wafugaji ili waweze kuingia katika soko, na kupanua sekta binafsi ili wawekeze katika kilimo.
Pili, tulijadili ripoti ya maendeleo ya dunia katika migongano, ripoti hii ina mambo muhimu ambayo yamefanikishwa na benki ya dunia na washirika wengine wa maendeleo katika hali isiyo nzuri na miji iliyoathirika na kutoelewana.
Tunaamini kuwa Benki inaweza kutumia nafasi yake kusaidia kupatikana kwa kazi na maendeleo ya sekta binafsi ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi,maendeleo imara kwa taasisi za fedha, na kuimarisha ulinzi na sheria, na kushawishi mabenki kuwa tayari kushiriki katika hatua za mwanzo za mitikisiko na migogoro inayoathiri taasisi zinazowahusu.
Eneo letu la mwisho tuliloliangalia lilikuwa ni kwenye maendeleo ya kuimarisha na kubadilisha kundi la benki ya dunia. Kwa kipekee tulikaribisha taasisi zisizokuwa rasmi za muungano wa kimataifa na kimaendeleo, pamoja na taasisi ambazo zinamulika taasisi hii ya fedha na zile zinazoangalia mtikisiko mpaya wa uchumi na maafa ya asili yasiyotarajiwa.
Pia tulikaribisha baraka za ongezeko la mitaji kwa benki za kimataifa kwa ajili ya kujenga upya maendeleo, na tunafarijika kuona kuwa michango halisi imeanza kuingia.
Tunasubiri kuona ongezeko la mitaji kwa mashirika ya kifedha na kundi la benki na sekta binafsi za kimaendeleo. Fedha zote hizo zitawezesha benki ya dunia kuendelea kuzisaidia nchi wanachama katika kupambana na umasikini.
Pia tulikaribisha kitendo cha kuweka muundo wa kundi la benki ya dunia katika utaratibu ambao utasaidia kuwajibika katika kazi za kila siku kwa wateja wake na kupata matokeo mazuri.
Tulikaribisha ripoti ya serikali na juhudi za mazungumzo yenye mipango ya kuimarisha utendaji kwa wadau na taasisi za fedha kwa ujumla. Bw. Al Khalifa alimalizia kwa kusema kuwa kuna mengi sana ya kusema lakini anaona aishie hapo.Katika mazungumzo hayo aliambatana na Rais wa Benki ya dunia ambaye ni Robert B. Zoellick, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la fedha la kimataifa Bw. John Lipsky na Bw.Richard Mills, ambaye ni Mkurugenzi Mawasiliano ya pamoja,Benki ya dunia.
No comments:
Post a Comment