
Na Mwandishi Wetu.
Shindano la kumsaka mlimbwende wa Kilimanjaro 2011 linategemewa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni baada ya waandaji wa shindano hilo kudai kuwa sehemu kubwa ya maandalizi imeanza kukamilika ikiwa ni pamoja na kuwakusanya warembo kutoka sehemu mbalimbali kwaajili ya mazoezi(catwalk).
Msemaji wa shindano hilo, Bw. Methuselah Magese amesema kuwa yeye na muaandaji mkuu wa shindano hilo Jaquekline Chuwa tayari wako katika mchakato mnene kuhakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu anatokea mkoani Kilimanjaro.
Shindano la Miss Kilimanjaro litafanyika june 11 katika hoteli ya Salsanero iliyoko shant town mjini Moshi ambapo mchekeshaji maaru wa kundi la Orijino Komedi,Masanja Mkandamizaji atakuwa ndiye MC wa siku hiyo wakati msanii 20% na wengine wengi wataburudisha vyakutosha.
Miss Kilimanjaro 2011 imedhaminiwa na Vodacom,Redd's,Africa Sana Pub,Rafiki Min Super Market,Excutive Solution,Bamm Solution na Uniqueentertz Blogspot.
No comments:
Post a Comment