HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 29, 2011

Misa ya kumuombea marehemu Mzee John Luwanda

Marehemu Mzee John Luwanda

Mzee wa Libeneke, Lukwangule, Beda Msimbe, anapenda kuiarifu jamii nzima ya wanalibeneke kwamba Misa ya kumuombea marehemu baba yake, John Luwanda, Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania, itafanyika katika kituo cha maombi cha Marian Faith Healing Centre, Riverside Ubungo Jumamosi Aprili 30, saa 12 asubuhi.

Misa hiyo itafuatiwa na upandaji wa Msalaba katika kaburi la Marehemu Goba Kibululu na kisha sadaka kidogo kwa watakaofika kuadhimisha upandaji wa Msalaba.

Nyote mnaoweza kufika mnaalikwa na wale wasioweza tuwe sote katika roho kwa sala.

Mungu ametoa, Mungu ametwaa Amina. Roho ya Marehemu John Luwanda na Marehemu wote zipumzike kwa amani Amina.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad