
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL),David Minja akizungumza leo kwenye semina ya waandishi wa habari za michezo iliyofanyika katika hoteli ya South Beach,Kigamboni jijini Dar.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari za michezo katika semina iliyoendeshwa leo kwenye hoteli ya South Beach,Kigamboni jijini Dar,ikiwa ni semina ya maandalizi ya Ligi ya Kili Taifa Cup 2011 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mei 6 katika mikoa sita hapa nchini.

Mkurugenzi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),Angetile Osiah akizungumza katika semina hiyo.

Ofisa Uhusiano wa TBL,Dorris Malulu akifungua semina ya waandishi wa habari za michezo iliyofanyika leo katika hoteli ya South Beach,Kigamboni jijini Dar.

Baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akikabidhi jezi ya timu ya Yanga kwa nahodha wa timu ya waandishi wa habari washabiki wa timu hiyo,Muhidin Sufiani leo mara baada ya kumalizika kwa semina ya waandishi wa habari za michezo.katikati ni Mkurugenzi wa TFF,Angetile Osiah

Mkurugenzi wa TFF,Angetile Osiah akikabidhi jezi kwa Amri Masari wa Simba.

Magambo muhimu kabla ya mechi.

Beki wa Yanga (timu ya waandishi wa habari wapenzi wa Yanga),Bashir Nkoromo akijaribu kuzuia mpira usiende langoni kwake.

mtanange ukiendelea.

Streika wa timu ya waandishi wa habari wanaoishabikia timu ya Simba,Said Makala akiwa katika harakati za kumtoka beki wa timu ya Yanga,Bashir Nkoromo.

...Hapa hapiti Mtu....

Fanya unavyoweza lakini hapa hupiti ng'ooo........
Kama Cristiano Ronaldo vileeeee......



Dochiiiiii la Maaaaaanaaaa.......
No comments:
Post a Comment