Tangu kuibuka kwa Babu wa Loliondo na dawa yake ya 'maajabu', ambayo inatibu ugonjwa wowote na ambayo haina gharama kubwa zaidi ya kusimama muda mrefu kwenye foleni ukisubiri zamu yako ya kupata kikombe, nimekuwa nikipata wakati mgumu sana mtu anaponiuliza iwapo dawa hiyo inatibu au la.
Nimekuwa nikipata wakati mgumu kwa sababu awali ya yote dawa hiyo haijafanyiwa utafiti wa kisayansi lakini pia hakuna sayansi iliyo juu ya miujiza ya Mungu. Babu wa Loliondo ameoteshwa juu ya dawa hii kwa hivyo siwezi kusema kwa hakika iwapo inaponya ama la. Pia hajatokea mtu ambaye naweza kuthibitisha kwa asilimia 100 kwamba amepona.
Lakini swali kubwa kabisa ambalo nimekuwa nikijiuliza ni hili, "Kama dawa hii si dawa mbona watu wameelekea Lolindo kwa makumi ya maelfu?" Wakati swali hili likiendelea kuzungukazunguka ubongoni mwangu nikagongana na makala hii kwenye mtandao, "Placebos Work - Even if Patients are in On the Secret". Tafsiri rahisi ya kichwa hiki cha habari ni hii, "Dawa Bandia Zinafanya Kazi - Hata Mgonjwa anapoambiwa kwamba Anapatiwa Dawa Bandia".
Makala hii iliandaliwa na Maureen Salmo wa gazeti la News Day. Maureen anasema alipofanya uchunguzi wake kuhusu nguvu ya madawa bandia kutibu magonjwa aligundua kwamba hata mgonjwa alipokuwa akielezwa kwamba anachopatiwa ni dawa bandia mgonjwa huyo bado alionesha kupata nafuu kubwa baada ya kutumia dawa hizo bandia, wapo waliopona kabisa.
Akipitia utafiti ambao ulijumuisha wagonjwa 80 waliokuwa wakisumbukiwa na vidonda vya tumbo aliona kwamba wagonjwa wahawa waligawanywa katika maundi mawili. Kundi la kwanza wakaelezwa wazi kwamba walichokuwa wakipatiwa kama tiba hakikuwa dawa halisi ya kutibu ugonjwa wao na lili kundi lingine halikupatiwa tiba kabisa. Baada ya majuma matatu kundi lile liliopatiwa dawa bandia walisema wamekuwa wakijisikia nafuu kubwa tofauti na wale ambao hawakutibiwa kabisa.
Maureen pia alithibitishiwa na Dr. Ted Kaptuchuk wa Chuo Kikuu cha Utabibu cha Havard, ambaye aliendesha utafiti huu, kwamba wale waliopatiwa dawa bandia sio tu kwamba walikuwa wakijisikia nafuu lakini vipimo vya hospitali vilionesha kwamba ugonjwa wao ulikuwa unatoweka kama vile ambavyo ungetoweshwa na dawa halisi.
Utafiti huu uliofanyika mwaka 2008 ulionesha kwamba nchini Marekani karibu asilimia 50 ya madaktari, kwa siri, huwapatia wagonjwa wao, wasiofahamu, dawa bandia.
Dr. Kaptuchuk anasema uchunguzi wake ulidhamiria zaidi kutazama nguvu ya dawa bandia kwa wagonjwa ambao wanaelezwa awali kwamba wanapatiwa dawa bandia, na sio kuwapatia dawa hizo kwa siri. Tafiti nyingi kabla ya huu wa daktari huyu zimethibitisha kwamba dawa bandia zimekuwa zikitibu magonjwa ya wagonjwa wasiofahamu kwamba wanapatiwa dawa bandia. Kufanya kazi kwa dawa hizi kunaitwa kwa kimombo, "Placebo Effect".
"Tulipokuwa tukifanya utafiti huu hatukutegemea matokeo haya. Tulitegemea kwa sababu wagonjwa wetu wanafahamu kwamba wanapatiwa dawa bandia basi hali zao zingekuwa mbovu zaidi. Lakini imekuwa kinyume, imetushangaza sana." Anasema Dr. Kaptuchuk.
Daktari huyu anaendelea kufafanua kwamba...
IMAN IMANI IMANI HATA WAHENGA WALISEMA IAMANI USHINDA KUDRA.MIMI NAKUBALIANA NA ILI KWA SABABU IMANI ZAWATU HASWA WANAPOTESEKA NA MARADHI KWA MDA MREFU MIOYO YAO INA KITU NGOJA NIJARIBU HII DAWA UWENDA NIKAPATA NAFUU HIYO SILKA YA BINADAMU AU KIUMBE HAI KINACHOSUMBULIWA
ReplyDeleteNAKUBALIANA NA HII DAWA NA SITOWAKATISHA TAMAA WALE WALIOKWENDA NA WANAOKWENDA KUNYWA USUSANI WANAPOMTANGULIZA MUNGU MBELE KWANI WAZUNGU WALIO WENGI HAWAAMINI MUNGU NA MTU ASIE AMINI MUNGU VITU KAMA HIVI KWAKE NI SOMO JIPYA KABISA
IMANI USHINDA KUDRA
Dunda