
Mambo vipi Mzee wa Mtaa kwa Mtaa,
Naomba uipandeshe hii picha ambayo nimekumbana nayo nikiwa katika pita pita zangu huku mitaa,huyu ni Dereva wa Daladala lifanyalo safari zake kati ya Mwenge - Posta akiwa amepiga mbonji katika foleni ya mataa na kujisahau kabisa kama yupo barabarani.
Hivi kwa Mwendo huu ajali za Barabarani zitamalizika kweli hapa mjini??
Mdau wa Mtaa kwa Mtaa.
No comments:
Post a Comment