Naibu waziri wa Ujenzi Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akifurahia jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Alli Iddi (katikati) na Mh. Zakia Meghji (Mbunge wa viti maalum, CCM) nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge leo mjini Dodoma kufuatia vurugu zilizotokea jana wakati wa zoezi la ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu uundwaji wa katiba mpya ambapo ametoa wito kwa serikali kuongeza muda zaidi wa ukusanyaji wa maoni na idadi ya mikoa ambayo itashiriki katika zoezi hilo.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hadji Mponda (katikati) akizungumza na Bw. Anic Kashasha (wa pili kutoka kushoto) mtendaji mkuu wa kampuni ya Tricy Solutions ya jijini Dar es salaam inayojihusisha na utoaji wa huduma na biashara ya vifaa vya umwagiliaji wa dawa za kuulia wadudu, Bajaj au Pikipiki maalum za kubebea wagonjwa na vifaa vya kuzimia moto leo katika viwanja vya Bunge Dodoma.

Mbunge wa Longido Mh. Michael Lekule Laizer akitelemka ndani ya pikipiki maalum ya kubebea wagonjwa aliyopewa na Waziri mkuu Mizengo Pinda kusaidia wananchi wa jimbo lake leo mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku (kushoto) akizungumza jambo na Mbunge wa Igunga Bw. Rostam Aziz (Kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.

Raia wa kigeni wakitoka ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma ambako walipata fursa ya kufuatilia mijadala ya wabunge.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
No comments:
Post a Comment