
Stamili John (kushoto) mkazi wa Kongwa mkoani Dodoma ambaye amelazwa katika Hospitali ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam akimshukuru Mratibu wa Programu kutoka Hands of Africa Foundation Joseph Magutu (kulia) mara baada ya kumkabidhi msaada wa mafuta ya kuzuia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Msaada huo ambao ni mafuta ya watoto na watu wazima wenye thamani ya shilingi milioni 8.2 umetolewa na shirika rafiki la Society for Threatened People la nchini Ujerumani utapelekwa kwa Albino wa mkoa wa Kilimanjaro pamoja na mikoa mingine jirani na wagonjwa wa saratani wenye ulemavu wa ngozi walioko katika Hospitali ya Ocen Road.
No comments:
Post a Comment