HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 18, 2011

naibu waziri wa viwanda na biashara atembelea TBS

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu( Katikati) akizungumza na wafanyakazi na waandishi wa Habari katika ziara yake ya kutembelea Shirika la Viwango nchini TBS. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBS Bw Charles Ikerege na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo Prof Apollinaria Pereka.
Naibu Waziri Nyalandu akitembelea maabara na maeneo mbali mbali katika ziara yake ya kutembelea Shirika la Viwango nchini TBS.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu katika Picha ya Pamoja na Viongozi na Maafisa wa Wizara yake na Shirika la Viwango nchini TBS mara baada ya kutimisha ziara ya kulitembelea shirika hilo.


******** *******

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, amelitaka Shirika la Viwango Nchini TBS kuongeza juhudi katika kusimamia ubora wa bidhaa nchini ili kuwapa watumiaji thamani halisi ya fedha wanazotumia katika kununua bidhaa hizo.

Naibu Waziri Nyalandu ametoa rai hiyo katika ziara yake ya siku moja ya kulitembelea Shirika la Viwango nchini TBS ambalo lipo chini ya Wizara yake.

“TBS mnalinda maisha ya watu, mnalinda mali zao, fanyeni kazi zenu kwa umakini mkubwa, bila woga, serikali haitawaingilia na badala yake, itawasimamia na kuwawezesha ili mtimize vyema majukumu yenu” alisema Naibu Waziri

Akimkaribisha Naibu Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw Charles Ikerege amesema, TBS imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kusimamia ubora wa bidhaa nchini licha ya uwezo mdogo wa kifedha ilionao na kuiomba serikali kuongeza fungu la fedha ili kulipa shirika hilo uwezo zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad