HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 17, 2011

Mh. Nyarandu apata ugeni toka UNIDO leo

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo ya Viwanda UNIDO Bw Emanuel Kalenzi (Kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu(Kulia). Wengine na Wakurugenzi katika Idara ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda na Biashara.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, leo amefanya mazungumzo mafupi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda UNIDO hapa nchini Bw Emanuel Kalenzi.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ya Naibu Waziri Nyalandu, na kuhudhuriwa na mkurugenzi wa Idara ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda na Biashara Bibi Eline Sikazwe na Mkurugenzi Msaidizi Mhandisi Elly Palangyo.

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yamejikita katika mipango na mikakati mbali mbali ya Wizara na Shirika hilo yenye nia ya kuongeza ufanisi wa sekta ya viwanda hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad