Mkurugrnzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford,Rashid Tenga (katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya makubaliano ya kuingia ubia na Kampuni ya Nuturn ya nchini Kenya katika hotel ya Movenpick,jijini Dar.wengine pichani toka kulia ni Jesse Munene,Mkurugenzi wa Nuturn, Alfred Amulyoto, Xolani Hitlana na Khavo Moyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford,Rashid Tenga pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Nuturn, Alfred Amulyoto wakitiliana saini za makubaliano ya ubia.
=== === === ===
=== === === ===
Kampuni maarufu nchini ya ‘Aggrey and Clifford’ inayojihusisha na biashara ya masoko jumuishi na mawasiliano leo imesaini mkataba na kampuni ya Nuturn kutoka nchini Kenya ambayo inajihusisha na biashara za matangazo na mawasiliano. Kampuni hizi mbili zimeingia ubia huu ili kusaidia kukuza ujuzi na kuongeza wigo wa huduma hizi kwa nchi zote mbili.
Kampuni zote mbili za ‘Aggrey and Clifford’ na Nuturn zinazijihusisha na shughuli za masoko jumuishi na mawasiliano zikiwa na uzoefu mkubwa na wa muda mrefu katika biashara hii.Ushirikiano huu utasaidia kuongeza uwezo wa makampuni haya kusaidia kukuza biashara na bidhaa kutoka nchi zote mbili kushindana kwa ufanisi zaidi katika masoko ya nyakati hizi.
Akiongea Mkurugenzi Mtendaji wa Aggrey and Clifford Bw. Rashid Tenga alisema “Ushirikiano huu utapanua wigo wa mitandao yetu. Sasa tutawezakusaidia wateja wetu kupanga mbinu za mpya za masoko, kuzindua huduma au bidhaa mpya na kufanya kampeni kubwa za kutafuta masoko na kurusha matangazo nchini kenya na Tanzania.
Kwa ushirikiano huu kampuni yetu imeongeza maarifa na uwezo wa utendaji hivyo kusaidia kampuni kupata ujuzi,zana,kukuza vipaji vya watendaji na rasilimali.Malengo yetu ya siku zijazo ni kuhakikisha na tunajenga msingi imara wa mafanikio makubwa kwa wateja wetu” alisema Bw Tenga
Aggrey and Clifford inarekodi ya kipekee katika uwanja wa matangazo na masoko jumuishi kwani ni kampuni ya kwanza kabisa nchini kuanziasha huduma ya matangazo kupitia mitandao ya simu kwa ushirikiano wa kampuni ya Push Mobile ambayo inashughulika na udhibiti wa taarifa za mitandao ya simu.Pia Kampuni ya Aggrey and Clifford ni kampuni ya kwanza kuanzisha na kuweka matangazo ya bidhaa na huduma za ndani ya nchi katika mfumo wa mitandao .
Kampuni ya Nuturn kampuni asilia ya kenya ambayo inatoa mbinu mpya za kwa wafanyabiashara wenye uwezo wa kutoa alama 360 za ufumbuzi wa mawasiliano, matangazo, vyombo vya habari na huduma za mahusiao na jamii. Kampuni hii inazaidi ya miaka 15 ya uuzaji wa kina wa mbinu za masoko na mawasiliano wakiwa wamejikita zaidi kubuni kampeni zenye mafanikio ambayo ndio hasa faida ilio wekezwa na mteja
Nuturn inashika namba tisa katika mtandao wa kampuni kubwa za masoko duniani kote ni ni mshirika wa WPI.Mbali na kuwa na uhusiano wa kimataifa , Nuturn ni mwanachama wa Chama cha Watendaji wa Matangazo na pia ni mdau wa Jamii ya Masoko ya kenya na Chama cha Mahusiano ya Umma ya Kenya.
No comments:
Post a Comment