Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imeweka hadharani majina matano ya baa zilizofuzu kuingia fainali ya shindano la kuchoma nyama kwa mkoa wa Dar Es salaam, lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma”
Akitangaza majina hayo, meneja wa Bia ya Safari Lager Bw. Fimbo Butallah alisema; Baada ya uzinduzi wa shindano la mwaka huu mwezi Februali, wananchi walitakiwa kupendekeza majina ya baa wanazopenda ziingie katika shindano kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia simu zao za mkononi. Zoezi hilo limeweza kutupatia majina matano yaliyopata kura nyingi zaidi kuliko baa nyingine katika mkoa wa dare s Salaam; na baa hizi ni;
Kisuma Bar – Temeke
Meeda Pub – Sinza
Gadafi Bar – Yombo
Titanic Bar – Vingunguti na
Fyatanga Bar – Tegeta
Hatua inayofuata ni majaji kuzitembelea baa hizi na kuzipatia mafunzo (semina) ya uchomaji bora wa nyama, na kufanya ukaguzi katika baa hizo, kisha baa hizi tano zitapambana katika uchomaji wa nyama siku ya Jumapili tarehe 13 Machi, katika viwanja vya LEADERS CLUB, kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 12 jioni ambapo mshindi atapatikana.
Akitaja zawadi za washindi, Butallah alisema; baa itakayoshika nafasi ya kwanza itajinyakulia shilingi Milioni Moja, mshindi wa pili, Laki Nane, Mshindi wa Tatu laki Sita, Nafasi ya Nne; Laki Nne na nafasi ya Tano shilingi Laki Mbili.
Butallah pia aliwaomba wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam wajitokeze siku hiyo ya Jumapili katika viwanja vya Leaders ili wajipatie Nyama iliyo bomba zaidi jijini Dar Es Salaam ikishushiwa na Safari Lager baridi.
Pia kutakuwa na burudani za kutosha zikiongozwa na Bendi maarufu ya African Stars “Twanga Pepeta”.
Mashindano ya mwaka huu yanafanyika katika mikoa mine ambayo ni; Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Arusha na Mbeya. Ambapo Mbeya imekamilisha fainali zake jumamosi iliyopita, na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro itakuwa mwishoni mwa mwezi Machi.
Vigezo vinavyoangaliwa na majaji katika mashindano haya ni pamoja na Usafi wa eneo, vifaa na muhusika, uchaguzi wa nyama, maandalizi ya nyama, jinsi ya uchomaji, muda unaotumika, jinsi nyama inavyofikishwa kwa mlaji na Ladha.
No comments:
Post a Comment