HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 16, 2011

BREAKING NYUZZZ: HUKO GONGO LA MBOTO HALI SI SHWARI USIKU HUU KUTOKANA NA MILIPUKO YA MABOMU

HALI SI SHWARI USIKU HUU HUKO MAENEO YA GONGO LA MBOTO,KWANI INASEMEKANA KUNA GHALA LA MABOMU KWENYE MOJA YA KAMBI ZA JESHI LA WANANCHI (JWTZ) LILILOPO MAENEO HAYO LINALIPUKA NA KUSABABISHA MILIPUKO MIKUBWA NA YENYE KUHATARISHA MAISHA YA WAKAZI WA MAENEO YA JIRANI NA KAMBI HIYO.

HADI HIVI SASA MILIPUKO HIYO INAENDELEA NA WAKAZI MAENEO YA JIRANI NA HAPO WAMELAZIMIKA KUYAACHA MAKAZI YAO ILI KUJINUSURU NA HALI HIYO INAYOENDELEA HIVI SASA.

HII NI MARA YA PILI KUTOKEA KWA TUKIO KAMA HILI HAA NCHI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA ISIYOPUNGUA MITATU ILIYOPITA,AMBAPO HAPO AWALI ILITOKEA MAENEO YA MBAGALA JIJINI DAR NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU NA WENGINE WENGI KUJERUHIWA VIBAYA NA KUACHWA NA VILEMA MPAKA HIVI SASA.

TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA,HIVYO TUVUTE SUBIRA NA TUOMBE DUA KWA BABA MUUMBA ILI ATUNUSURU NA JANGA HILI.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad