Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami, ameondoka nchini kuelekea nchini India kwa ziara ya siku saba ili kuhudhuria mkutano wenye lengo la kuhamasisha Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na India.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kuondoka, Waziri Chami amesema, nia ya serikali ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na nchi rafiki pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini. Amesema akiwa nchini India, atazungumza na wafanyabiashara na taasisi mbali mbali za kibishara nchini humo ili ziweze kuja Tanzania kujionea fursa zilizopo na kuwekeza, hususan katika mamlaka ya EPZA.
Katika ziara hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya Kamal Steel ya India yenye miradi mbali mbali nchini Tanzania, Waziri Chami ameongozana na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya EPZA Dkt A. Meru. Ziara hiyo itamwezesha Mh Waziri kuhudhuria Mkutano wa kimataifa ujulikanao kama Global Commerece Chambers of Maharashtra utakaofanyika katika mji wa AURANGABAD katika jimbo la MAHARASHTRA.
No comments:
Post a Comment