HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 25, 2011

sauti za busara kuja kivingine mwaka huu


Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara,Yusuf Mahmoud akizungumza katika mkutano wa ufunguzi rasmi wa tamasha hilo kwa vyombo vya habari asubuhi hii katika hoteli ya Southen Sun,jijini Dar.kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel,Brian Karokola,Makamu Mwenyekiti wa Tamasha hilo,Simai Said (pili kulia) na kulia ni Nahaat Mahfoudh kutoka Zantel.
Makamu Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti Za Busara,Simai Said akiwakaribisha wanahabari na wasanii katika mkutano wa ufunguzi wa tamasha hilo kwa wanahabari na wasanii leo katika hoteli ya Southen Sun,jijini Dar.wengine ni Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti Za Busara,Yusuf Mahmoud,Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel,Brian Karokola Meneja wa Tamasha la Sauti za Busara,Stella Stephen.

Sauti za Busara ni moja ya matamasha yenye mvuto wa kipekee barani Afrika, mwaka huu litafanyika kwa mara ya nane visiwani Zanzibar katika Mji Mkongwe kuanzia Februari 9-13.
Tamasha hili hukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali na kuwaweka pamoja, wakisheherekea na kufahamiana kama alivyosema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya ufunguzi wa tamasha la mwaka 2010.

“tukio hili ni muhimu kwa kuwa linatoa fursa kwa wageni na wenyeji wa tamaduni mbalimbali kubadilishana mawazo,kuonyeshana upekee wao, utajiri na utofauti wa muziki wetu. Kwa ujumla linachangia kuimarisha muingiliano wa tamaduni na urafiki.”

Sauti za Busara huwakutanisha wasanii wakubwa wa muziki barani Afrika pamoja na kuibua vipaji vingine nchini. Mwaka huu vikundi 40 vitatumbuiza, baadhi ni, Orchestre Poly Rythmo de Cotonou (Benin), Blick Bassy (Cameroon), Otentikk Street Brothers (Mauritius), African Stars Band aka Twanga Pepeta (Tanzania), Mlimani Park Orchestra (Tanzania), Kwani Experience (South Africa), Culture Musical Club (Zanzibar), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta ft. Bi Kidude (Zanzibar), Jagwa Music (Tanzania), Bismillahi Gargar (Kenya), Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar), Djeli Moussa Diawara (Guinea), Christine Salem (Reunion), Yaaba Funk (UK), Muthoni The Drummer Queen (Kenya), Jahazi Modern Taarab (Tanzania), Les Frères Sissoko (Senegal), Sukiafrica Sukiyaki Allstars (Pan Africa / Far East), Groove Lélé (Reunion), Vusa Mkhaya & Band (Zimbabwe / Various), Djaaka (Mozambique), Nomakanjani Arts (Zambia), Percussion Discussion Afrika (Uganda), Tunaweza Band (Tanzania), Staff Band Namasabo (Tanzania), Lelelele Africa (Kenya), Atemi & the Ma3 Band (Kenya), Sauda (Tanzania).

Sherehe za mwaka huu zitafunguliwa na maonyesho mbalimbali ya kuvutia, muziki wenye nakshi mbalimbali ikiwemo nyimbo za kiswahili, madansa, maonyesho ya vipande vya filamu za muziki kutoka Tanzania, Uganda, DRC, Ivory Coast na Senegal.

Wakati huohuo, tamasha litadhamini Busara Xtra, yaani matukio ya nje ya tamasha yatakayoandaliwa ndani ya Zanzibar na ambayo yatawavutia na kuwanufaisha wageni waalikwa.
Hii itatoa fursa kwa wasanii wa ndani kuonyesha kazi zao, kuwahamasisha wageni kuendelea kutazama maeneo mengine ya visiwa na kuongeza kipato kwa watu wengi.

Vilevile watu 25 watanufaika kwa kupata mafunzo ya kitaaluma ya sauti (live sound engineering), jukwaa na sanaa ya habari.

Pamoja na kuongeza pato la taifa, zaidi ya watanzania 100 huajiriwa katika tamasha hili kila mwaka, vilevile hukuza na kuhifadhi muziki na tamaduni za Visiwa vya Zanzibar.

Sauti za Busara imeufanya muziki kutoka pande zote za Afrika ukubalike na kujulikana, imedumisha amani na ushirikiano mzuri katika jamii, kutangaza tamaduni za Afrika Mashariki na kuimarisha sekta ya utalii .

Hakutakuwa na kiingilio kwa wakazi wa Afrika Mashariki kuanzia jioni hadi saa kumi na mbili za jioni na watakaoingia kuanzia wakati huo watatozwa shilingi 2000 za kitanzania. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu www.busaramusic.org

Busara ni taasisi isiyo ya kiserikali inayodhaminiwa kwa mwaka mzima na ubalozi wa Norway.
Hali kadhalika, tamasha la Sauti za Busara lisingefanikiwa pasipo ushirikiano mkubwa kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Zantel ambao ndiyo wadhamini wakuu.

Wengine ni HIVOS, Goethe Institut, US Embassy, ACP music festival network, Culturesfrance, Memories of Zanzibar, Gallery Tours, Zanzibar Grand Palace Hotel, Grand Malt, British Council, Azam Marine, Fly 540, ZG Films, Zanlink, SMOLE II, Southern Sun Hotel, Radio Times FM , Tabasam tours… na watu wote wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad