
Mshindi wa Pili wa sgindano la Tusker Project Fame4 2010 ambalo limefikia tamati hivi karibuni,Peter Msechu akiwa ndani ya studio za Clouds Fm 88.4 leo jioni ndani ya kipindi cha XXL akifanyiw amahojiano mafupi na B Dozen kuhusiana na mchakato mzima wa shindano hilo na hatma ya yeye kuibuka mshindi wa pili.

Peter akiwa amepozi na Mwendesha kipindi cha XXL,B Dozen pamoja na Adam Mchovu (shoto).baada ya kufanya mahojiano yao mafupi.

Peter Msechu akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Clouds Media Group pichani kati,Joseph Kusaga kwa kumpa maneno ya ushauri na yenye kumtia moyo katika kuinedeleza fani ya muziki hapa Tanzania.

Peter Msechu akiwa ndani ya ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Clouds Media Group pichani kati,Joseph Kusaga jioni ya leo mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo.Kushoto ni Meneja bidhaa wa kampuni ya Serengeti Nandi Mwiyombela. Joseph Kusaga a.k.a Joe nae alimpa maneno ya kumjenga kwamba amefanya juhudi kubwa sana mpaka kufikia hapo,kikubwa asidhani ndio amefika,safari yake bado ni ndefu hivyo anahitaji kujituma zaidi katika kukiendeleza kipaji chake cha muziki.
No comments:
Post a Comment