
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare akiamkabidhi zawadi mtoto yatima Rahma wa kituo cha Umra kilichopo Magomeni ,kwenye kampeni ya share & care itakayofanyika Tanzania nzima kwa mwezi huu wa Decemba,aliyembeba mtoto Meneja udhamini wa kampuni hiyo Rukia Mtingwa.

Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Edwin Temba akikabidhi sabuni na vitu mbalimbali kwa watoto yatima wa kituo cha kuwama kilichopo sinza kwenye viwanja vya leaders club kwenye kampeni ya share & care iliyoandaliwa na Vodacom Foundation.

Mfanyakazi Geoffrey Wilfred wa kitengo cha kuhudumia wateja wa Vodacom Tanzania akiwakabidhi mbuzi watoto wa Yatima Trust Fund cha mbagala kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu , kampeni ya share & care itaendelea kufanyika Tanzania nzima kwa mwezi huu wa Decemba .

Wafanyakazi wa kitengo cha New Technology wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha New Life cha Mburahati.

Mfanyakazi wa Vodacom kitengo cha rasliamali watu Solomon Rwagombwa akikabidhi maziwa ya kopo na vitu mbalimbali kwa watoto yatima wa kituo cha kuwama kilichopo sinza kwenye viwanja vya leaders club kwenye kampeni ya share & care iliyoandaliwa na Vodacom Foundation

Mtoto Miriam Chirwa akiwaburudisha watoto yatima 600 waliofika kwenye viwanja vya leaders club kwenye kampeni ya share & care iliyoandaliwa na Vodacom Foundation.
No comments:
Post a Comment