
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Bi. Elizabeth Missokia (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za HakiElimu juu washindi wa Shindano la Insha na zawadi walizopewa,(katikati) Meneja Idara ya Upatikanaji habari HakiElimu Bw. Robert Mihayo (kulia) Mdhamini wa muungano wa vituo vya walimu Tanzania Dr. Swai Fulgence
************* *****************
Na. Mwandishi wetu
Haki Elimu kwa kushirikiana na Taasisi ya Vituo vya walimu Tanzania (TRCC) imetangaza rasmi washindi wa shindano la Insha/ Michoro walioshinda katika uhandishi wa Insha ya “ Mafunzo ya Walimu Kazini yana Umuhimu Gani Katika Kuboresha Elimu Tanzania” ambapo washindi hao wamepata zawadi mbalimbali kulingana na ushindi wao.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Haki Elimu Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji Haki Elimu Bi. Elizabeth Missokia amesema washindi wawili wa kwanza wamejinyakulia kiasi cha Shilingi 500,000/= kila mmoja na radio moja ambao ni Noela Nyabatake kutoka Shinyanga na Bihemo Dawa Mayegela kutoka Mbeya na Washindi wengine 10 waliojinyakulia kiasi cha shilingi 200,000/= na radio moja kila mmoja ambao nao ni Irene Ndomi Cartoonist kutoka Dar es Salaam na Farai Alfred Sulul kutoka Iringa.
Aidha Bi. Elizabeth amesema watu 901 wenye umri kati ya miaka 9 na 80 walishiriki katika shindano hilo kati yao wanawake ni 224 sawa na asilimia 25 na wanaume ni 514 sawa na asilimia 57 ambapo asilimia 18 ya washiriki hawakuonyesha jinsia zao katika mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani ambapo pia amesema washiriki wa shindano hili walielezea umuhimu wa mafunzo ya walimu kazini kuwa huwasaidia kuborehsa taaluma yao ya ufundishaji, kuongeza maarifa juu ya mabadiliko ya mitaala, Kisayansi na Ujuzi wa Kazi, pia kuwawezesha walimu hao kupambana na Changamoto za Kitaaluma na Maisha kwa Ujumla.
Akihitimisha Bi. Elizabeth amesema Haki Elimu inaamini kuwa mwalimu bora ni kiungo muhimu katika kuboresha maendeleo ya Elimu katika kujenga msingi imara wa mafunzo bora pale anapokuwa katika kituo chake cha kazi kwa muda mrefu bila kujiendeleza na huku kukitokea mabadiliko ya mara kwa mara katika mitaala ambapo amesema ni muhimu mara baada ya mwalimu kuhitmu mafunzo ya ualimu kupata fursa ya kujiendeleza kwa kujisomea vitabu, kutumia vyanzo mbalimbali vya habari kama magazeti, radio, televisheni na kuhudhuria kozi fupi.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Bi. Elizabeth Missokia akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za HakiElimu juu washindi wa Shindano la Insha na zawadi walizopewa,(katikati) Meneja Idara ya Upatikanaji habari HakiElimu Bw. Robert Mihayo (kulia) Mdhamini wa muungano wa vituo vya walimu Tanzania Dr. Swai Fulgence
No comments:
Post a Comment