HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 4, 2010

TBL Yatoa Vifaa Vya Usalama Barabarani Kwa Jeshi La Polisi Leo

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, Editha Mushi akikabidhi fulana na stika za usalama barabarani Afisa Mnadhimu wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani,ACP Johansen Kahatano katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Trafiki jijini Dar.ACP Johansen Kahatano alipokea msaada huo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga.
Afisa Mnadhimu wa Polisi kikosi cha usalama barabarani, ACP Johansen Kahatano akionyesha baadhi ya stika zilizotolewa na kampuni ya bia TBL leo.
Askari wa usalama Barabarani,PC Faustina Ndunguru akibandika stika katika moja ya magari yaliyosimamishwa na kupandikwa stika hizo huku Meneja Mawasiliano wa TBL,Edith Mushi akiangalia.


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imekabidhi vifaa mbalimbali kwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano hayo jijini Dar es salaam Meneja mawasiliano wa TBL Bi Edith Mushi alisema Tbl imeona kuna umuhimu wa kutambua juhudi za Jeshi la polisi hasa kitengo cha usalama barabarani katika juhudi zake za kupambana na hali ya usalama barabarani hivyo tumeamua kutoa msaada wa baadhi ya vifaa ambavyo tunaamini vitasaidia kwenye juhudi hizo.

Bi Mushi alisema msaada huo kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani unatokana na TBL kutambua umuhimu wa usalama hivyo tunaamini vifaa hivi vitasaidia katika juhudi za kikosi hicho kwenye kusimamia sheria na taratibu za usalama barabarani.

Aidha aliwataka wenye vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu kwa pamoja kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani ili kuhakikisha ajali zisizo za lazima zinaepukika kwa kipindi chote”Ajali za barabarani zimekuwa chanzo kikubwa cha vifo na vilema kwa jamii ya kitanzania ajalinyingi zinachangia kuzorotesha maendeleo ya nchi yetu hivyo sote kwa pamoja tuungane kupinga ajali zisizo za lazima “alisema bi Mushi.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na fulana za mduara mia tano,Fulana na kola mia tatu stika maalumu zenye maelekezo mbalimbali ya mambo ya usalama barabrani mia tano, Vifaa vyote hivyo vina ujumbe juu ya matumizi salama ya barabara nchini Tanzania.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya mkuu wa kikosi cha usalama barabarani ACP Johansen Kahatano aliishukuru kampuni ya bia nchini kwa juhudi kubwa inayofanya kwenye jamii ya Watanzania na kuahidi kuvitumia vifaa hivyo kwenye kampeni mbalimbali za kuhamasisha jamii juu ya usalama barabarani.

Kamanda Kahatano alisema kutolewa kwa vifaa hivyo na TBL ni ishara tosha kwamba inawajali watanzania na vifaa hivyo vitakuwa chachu ya mapambano ya ajali zisizo za lazima nchini hasa kwa kipindi hiki cha wiki ya nenda kwa usalama barabarani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad