Mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mh. Hussein Mwinyi akikabidhi kombe la ushindi kwa muwakilishi wa kampuni ya Sigara Tanzania,Simon Maha mara baada ya kutangazwa washindi wa tuzo za Chama Cha Waajiri Tanzania (Association of Tanzania Employers) zilizotolewa jana katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar.
Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana,Mh. Juma Othman Kapuya akikabidhi kikombe cha ushindi wa pili kwa muwakilishi wa benki ya Standard Chartered katika hafla ya utoaji tuzo kwa makampuni yaliopo nchini. tuzo hizo zilitolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (Association of Tanzania Employers) jana katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar.
Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Nchini,Adv. Cornelius Kariwa,akikabidhi kikombe na cheti cha ushindi wa tatu kwa muwakilishi toka BP Tanzania.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mawasilano wa TBL,Steven Kilindo akifurahia ushindi walioupata wa Taaluma ya Afya na Usalama (Occupational Health and Safety) katika hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika jana usiku katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar.
Wafanyakazi wa TBL wakifurahia Tuzo yao waliyoipata.toka kulia ni Lilian Erasmus, Steven Kilindo (Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mawasiliano),Stephen Kolimba,Rosedomina Swai,Lilian Makau na Sarah Zayumba
Mdau Alfred Martin wa PPF (kulia) akikabidhi kikombe pamoja na cheti cha ushindi kwa mwakilishi wa kampuni ya Sigara Tanzania,Victor Kimaro ambao ndio walionyakuwa vikombe vingi katika tuzo hizo.
Wafanyakazi wa kampuni ya Sigara wakiwa na Vikombe vyao vya ushindi
washindi woote walipata picha ya pamoja na Mgeni rasmi.
Thursday, July 1, 2010

Home
Unlabelled
Tuzo Za ATE ,Kampuni Ya Sigara Yanyakua Ushindi
Tuzo Za ATE ,Kampuni Ya Sigara Yanyakua Ushindi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment