Dar ss Salaam. Lengo la jumuiko hili ni kuhamasisha ushiriki wa wanasayansi vijana katika shughuli za kisayansi hapa nchini kama nyenzo ya kupambana na umasikini na kukuza uchumi.
Mkutano huu utajumuisha kuzindua rasmi mtandao wa wanasayansi vijana Tanzania (utakaojulikana kama YES Network Tanzania), tovuti pamoja na jarida la mtandao.
Pia, jumuiko hili litakuwa ni jukwaa kwa wanasayansi vijana kubadilishana uzoefu- mafanikio na changamoto, kujadili na kutoa maazimio kwenye masuala mbalimbali yanayoikabili jamii ya watanzania katika mada mbalimbali kama vile mabadiliko ya tabianchi, sayansi na uvumbuzi, uhifadhi wa mazingira, usimmamizi wa rasilimali asilia pamoja na afya. Yote haya yatafanywa kupita tafiti mbalimbali walizozifanya.
Mkutano huu utajumuisha viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wadau wa sayansi nchini kutoka Wizara ya Sayansi Teknolojia na Mawasiliano, Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali.
No comments:
Post a Comment