
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunja akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya wajasiriamali kwenye kongamano la Wajasiriamali linalozungumzia mambo mbalimbali ya wajasiriamali katika kuchangia maendeleo ya nchi, lakini pia wajasiriamali hao. kubadilishana mawazo na uzoefu katika biashara zao ili kuifikisha mbali zaidi sekta ya kiuchumi, kupitia wajasiriamali na kuwaletea maendeleo. Kongamano hilo linakwenda pamoja na maadhimisha ya siku ya wajasiriamali na maonyesho ya taasisi mbalimbai za kibiashara na yafanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, katika picha katikati ni Bw. Paul Mashauri Mratibu wa maonyesho hayo na kulia ni Juliet Mwinuka Meneja Mradi.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo mara baada ya kuzindua maonyesho hayo kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara B. Joyce Mapunja akifungua kongamano hilo kwa hotuba, kulia katika picha ni Rais wa shirikisho la wafanyabiashara wenye Viwanda TCCIA Elvis Musiba.

Washiriki mbalimbali wa kon gamano hilo wakimsikiliza Katibu mkuu Viwanda na Biashara alipokuwa akitoa hotuba yake

Akina mama pia wamekuwa mstari wa mbele katika kongamano hilo kama unavyowaona wakiwa na makabrasha yao na kufuatilia kwa makini kila kilichoendelea.

Mjasiriamali na mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali kushoto alikuwepo katika kongamano kama unavyomuona akifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Bi Joyce Mapunja hayupo pichani.
(picha na John Bukuku/Full Shangwe Blog)
Kumradhi:
Ndugu wadau naombeni radhi sana kwa kukosewa kwa jina la Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunja.kwani mwanzo niliandika Bi. Blandina Nyoni.Nawashukuru sana wadau walionirekebisha katika hilo ma pia naombeni radhi sana kwa usumbufu uliojitokeza.
Ahsanteni.
PamoJah Katika Libeneke
Othman Michuzi.
jamani nimevutiwa na blog yenu lakini napenda kuwasahihjisha kidogo huyo katibu anaitw joyce mapunjo asanteni
ReplyDeletejamani nimevutiwa na blog yenu lakini napenda kuwasahihjisha kidogo huyo katibu anaitw joyce mapunjo asanteni
ReplyDeleteKaka tafadhali fanya masahihisho acha kupotosha jamii..Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko na Katibu mkuu ni Bi Joyce Mapunjo please she is not Blandina Nyoni..Nimesikitika sana. Cross check what you post before posting to be in safe side
ReplyDeleteteh teh, oyaaa, Othman, umekosea tena, umeandika 'Mapunja' ni 'Mapunjo' mwishoni hapo pana 'O' na siyo 'A' teh teh, unalo! Kazi eeh? Usikonde mwana, wala usijisikie vibaya, hutokea(ga).
ReplyDelete