HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 10, 2010

Fiesta Jipanguseee A-Town ni Mpango Mzima

Msanii wa muziki wa Hip Hop bongo Mwana FA akikamua jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha kubwa la Serengeti Fiesta Jipanguse 2010 ndani ya Matongee Club,mjini Arusha
Mzee wa Mwanza Mwanza Fid Q akishushu vina mwanzo kati na mwisho mbele ya wakati wa A-Town usiku wa kuamkia leo ndani ya tamasha la Fiesta jipanguse 2010.
Wasanii kutoka Kiumeni Wanaume TMK wakilishambulia jukwaa vilivyo
Mtoto wa Mama Said kutoka Wanaume TMK,Chege akiwaimbisha washabiki wake mpango mzima wa mambo bado ndani ya Fiesta Jipanguse 2010,tamasha hilo ambalo mdhamini mkuu ni kampuni ya Bia ya Serengeti breweries Ltd
Msanii kutoka THT atambulikae kwa jina la Mataluma akiwachezesha mchiriku wakazi wa A-Town waliojitokeza kwa wingi ndani ya Fiesta jipanguse 2010
Mwasiti akiwaimbisha washabiki wake wimbo wa kisa pombe ambao ulionekana kuwavutia vilivyo.
Msanii anaejivunia kutoka Morogoro Belle 9 akiimba jukwaani
Mr Misifa a.k.a Brazamen Dully Sykes akionesha mikogo yake mbele ya wakazi wa A-town ndani ya tamasha kubwa la Fiesta Jipanguse 2010.
Kidumu akionyesha umahiri wake wa kupiga vyombo.
Mwamba wa Kaskazini Joe Makini ukitesa nyumbani .
Mwanamuzi mkongwe wa muziki wa dansi Ndandaa Kossovo kulia na skwadi lake zima wakitumbuiza katika Fiesta Jipanguse 2010 usiku wa kuamkia leo ndani ya Matongee Club jijini Arusha. Mashabiki wa A-Taun wakijipangusa na Fiesta 2010Wasanii wa muziki wa Hip hop wajulikanao kwa jina la Wazushi wakikamua jukwaani usiku wa kuamkia leo ndani ya Matonge Club kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 mjini Arusha.
Wakazi wa Arusha waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 ndani ya Matongee Club usiku wa kuamkia leo.Tamasha hilo mdhamini wake mku akiwa ni kampuni ya bia ya Serengeti a.k.a mflame wa raha kamili yenye kudumu zaidi .Tamasha hili leo liko ndani ya Mji wa Moshi.

KWA PICHA ZAIDI ZAMA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad