HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 19, 2010

Big Brother Yaanza Rasmi Leo,mwisho na tatiana watinga tena


washiriki wa Big Brother All Stars wakiingizwa mjengoni kuanza safari yao ya kusaka dola milioni 200,000 atazopewa mshindi baada ya kukaa humo kwa muda wa siku 91.
Baada ya kuingia mjengoni ambapo haruhusiwi mtu mwingine kuingia, waliohudhuria uzinduzi walioneshwa kinachojiri kupitia bonge la luninga. hapo anaonekana Mwisho Mwampamba akiingia wa kwanza mjengoni. Pia alikuwa wa kwanza kutambulishwa baada ya waandaaji M-Net na DSTV kuficha majina ya washiriki hadi dakika ya mwisho. Mara tu baada ya kuingia mjengoni Mwisho
alionekana akiongea na Tatiana wa Angola kwa muda kiasi... Kisha wakakumbatiana kwa furaha... Limo iliyokuwa ikiwaleta washiriki mmoja baada ya mwingine.

Listi kamili ya washiriki 14 toka nchi 14 walioingia mjengoni usiku huu ni: Mwisho (Tanzania), Jen (Msumbiji) Code (Malawi), Hannington (Uganda), Kaone (Botswana), Lerato (South Africa), Meryl (Namibia), Munya (Zimbabwe), Sami (Ghana), Sheila (Kenya), Uti (Nigeria) na Yacob (Ethiopia), Paloma (Zambia) na Tatiana (Angola)
mwisho akiwa na jen wa Msumbiji na Paloma wa Zambia

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad