HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 21, 2010

Tamasha La Mtemi Mirambo Tabora

Meneja wa TBL,Fimbo Butallah pamoja na Mratibu wa Tamasha hilo,Amos Mkonga wakionyesha vipepetushi vinavyoelezea Tamasha hilo kwa waandishi wa habari waliofika katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo

TAMASHA LA MTEMI MIRAMBO TABORA

Chief Promotions imeandaa Tamasha la Ngoma za utamaduni liitwalo MTEMI MIRAMBO,lenye lengo la kukuza sanaa na kuvitangaza vikundi vya ngoma vilivyopo katika mkoa wa Tabora.

Tamasha hilo litaanza kufanyika katika viwanja vya chipukizi Tabora kuanzia Tarehe 16 - 18 Julai,2010 kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Siku hiyo shughuli mbali mbali zitafanyika kama vile maonyesho ya ngoma za asili,Sarakasi,Ngonjera na Nyakula vya asili.mgeni rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Moshi Mussa Chang'a.

Tamasha hili linakuja kwa udhamini mkubwa toka kwa kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Balimi,Bodi ya Utalii (TTB),Zain Tanzania na Merina Investment.

Chief Promotions imesajiliwa mwaka 2003 na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Baadae Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,na imefanya kazi na Mashirika mengi tu yakiwemo ya Umoja wa Matiaifa (UNAIDS,WHO,UNDP) na pia imefanya kazi na TBL,NSSF,TACAIDS na mengine mengi.

kwa mawasiliano
Amos Mkonga,
Mkurugenzi Mtendaji,
0755 638004/0655 638004

1 comment:

  1. Natafuta mkopo binafsi si wa benki - ntatoa na riba - nipo Dar

    ReplyDelete

Post Bottom Ad