HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 2, 2010

Siku Ya Mazingira Duniani

Mkurugenzi wa Mauzo wa TBL,Nik Broks (kulia) akiwa sambamba na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja wakitoa uchafu uliopo katika mtaro uliopo kando kando ya Kampuni hiyo ya Bia ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Mazingira dunia iliyoadhimishwa leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia TBL,Robin Goetzsche akijumuika pamoja na wafanyakazi wake katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani.Mkurugenzi huyo alishiriki bega kwa bega na wafanyakazi wake pamoja na wakazi wa eneo hilo kuhakikisha eneo lote la jengo hilo na maeneo ya jirani yanakuwa safi.
Mkuu wa Maswala ya utawala wa TBL,Phocus Lasway (kushoto) akiwa pamoja na Meneja wa Safari Lager,Fimbo Butallah (pili kulia) pamoja na wafanyakazi wengine wa TBL wakishirikiana kufanya usafi leo ikiwa ni siku wa Mazingira Duniani.
Da' Lilian Erasmus wa TBL akikabidhi baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi wa mazingira kwa Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Richard Mfugale ikiwa ni siku ya Mazingira Duniani iliyoadhimishwa leo Duniani kote.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiendelea na usafi leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad