HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 14, 2010

Miss Tanga Kufanyika June 19

MASHINDANO ya urembo Tanga, Miss Tanga 2010 yanaandaliwa na kampuni yetu ya Five Brothers Entertainment yenye maskani yake mjini Tanga.

Mashindano haya yanachukua nafasi yake baada ya vitongoji mbalimbali vya Tanga kumalizika, tumekusanya krimu ya warembo bomba waliokamilika kila idara kutoka Miss Lushoto, Miss Pangani, Miss Handeni, Miss Centeral, Miss Usagara, Miss College, Miss Chumbageni na Miss Ngamiani, katika kambi moja ya Miss Tanga 2010 iliyoanza tarehe 07 mwazi Mwezi huu hadi sasa.

Warembo hao wanaendelea kunolewa na walimu wao, ambao ni Miss Tanga 2009 Glory Chuwa na Amina Sadiki na Maryam Bandawe, Miss Tanga wa miaka iliyopita.
Lengo letu hasa ni kuboresha mashindano haya kuwa katika kiwango cha kimataifa, kama kauli mbiu yetu mwaka huu isemavyo, ‘Shindano Maridhawa,- A Wonderful Event, mtangundua hapo baadaye kuwa shindano letu tutalifanya katika mandhari ya kipekee, pembezoni ya ufukwe wa bahari, huku pepo zikivuma katika eneo la tukio hivyo kulifanya shindano la mwaka huu kuwa na msisimko wa aina yake.

Mbali na kuboresha Shindao, Safari hii pia tunampango kabambe wa kutoa wawakilishi walioandaliwa vema na wataoweza kutoa changamoto katika mashindano ya miss Tanzania na hata dunia.

Ni kweli tumedhamiria kulichukua taji la Taifa na mrembo wetu kufanya maajabu ambayo hayajawahi kufanywa katika mashindano ya urembo, Miss World 2010.

Mabibi na Mabwana, Fainali za mashindano ya Miss Tanga 2010 zitafanyika Juni 19 Jumaamosi ijayo, katika Hoteli ya Kifahari TANGA BEACH RESORT ambapo zaidi ya warembo 22 watachuana kuwania taji hilo.

Kupitia mashindano hayo pia tuna mataji mbalimbali kushindaniwa kama Miss Talent, Media choice award, Miss Photogenic na Miss Popularity.

Shindao hilo litaongwa za burudani ya wasanii wakali wa hapa Bongo, Ambao tayari tumeshafanya nao makubaliano mpaka sasa ni pamoja na msanii mahiri wa bongo fleva Matonya, Mc Babu Ayoub, Benjamin wa Mambo Jambo, na Ney wa Mitego na wengineo.

Kwenye upande wa zawadi tumepanga kuzitangaza rasmi alhamis, lakini tunachoweza kuwaambia sasa ni kwamba tumeboresha suala la zawadi kwa mwaka 2010 na kwamba Tumedhamiria kutoa zawadi ambazo tunaamini zinakuja kubadilisha maisha ya hawa warembo.

Mpaka hapa tunapenda kuwashukuru sana wadhamini ambao tayari wamekwisha jitokeza ambao ni Vodacom Tanzania, Redds Premium cold, ambao ndio wadhamini wetu wakuu, CRDB Bank-Tanga Branch, Hotel Kola Prieto, Sofia Productions, Vayle spring, Mrashan Investment, Breez FM, Aurora security, Amani Spring Water, DTP, Clouds FM, Tanga Beach Resort, Regal Naivea Hotel na Allan Light.

Mwisho kabisa tungependa kutoa shukuru za dhati kwenu ninyi waandishi wa habari, wadau mbalimbali walioshirikiana nasi kwa namna moja ama nyingine, wadhamini, Kamati ya Miss Tanga, Kamati ya Miss Tanzania, Waandaaji wa vitongoji mbalimbali vya Tanga, Walimu, bila kuwasahau mashabiki na yeyote ambaye ingestahiki kupata pongezi hizi, japo kimya kimya.

Tunakukaribisheni sana, kushiriki nasi katika kuipa Tanga ramani yake na heshima inayostahili, hapa Tanzania na duniani kote. Ahsante sana na karibu!

NAS ES COBERMKURUGENZI FIVE BROTHERS ENTERTAINMENT

Kampuni yetu ya Five Brothers Entertainment, kampuni hii inahusika na utayarishaji wa matamasha mbalimbali. Tunao uzoefu wa kutosha katika shughuli hizi hapa nchini na hii ni fursa adimu na muhimu kwa wadhamini kushiririkiana nasi kama watataka kujitangaza ama kufanya kazi nasi.

Inaweza pia kuwa fursa ya kubadilishana uzoefu, kufahamiana na pia kupata kazi za matunda ya kampuni yetu. Huu ni wito na mwanzo mwema wa kujenga ushirikiano wetu kwao wadhamini na kwao kwetu.

Tunaacha njia zetu za mawasiliano wazi kwa yeyote anayetaka kudhamini na kufaidika na mpango huu, ...
anaweza kuwasiliana nasi kupitia simu nambari:
0713 711413/0713 256 884
Kwa barua,
andika:-
Kwa Mkurugenzi,
5brothers Entertaiment,
P.O.Box 1254 Tanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad