HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 29, 2010

KCB yatoa punguzo la bei ya hisa

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Joram Kiarie, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi na kutambulisha huduma mpya yakutoa punguzo la bei ya Hisa kwa wanahisa wa benki hiyo, na mtandao wa kutoa huduma kwa wananchi wa Afrika Mashariki na Kati, ambapo mteja wa benki hiyo anaweza kutoa pesa za nchi aliyopo.

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

BENKI ya KCB Tanzania imezindua promosheni ya kuuza baadhi ya hisa zake chini ya bei ya awali lengo likiwa ni kukuza kiwango cha mtaji wa kampuni hiyo kubwa kanda ya Afrika Mashariki ikiwa rasilimali za dola za Kimarekani 2.6.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uuzaji huo wa hisa mshauri wa masuala ya kibiashara wa benki hiyo Amish Gupta alisema kwamba mpango huo mahususi umekuja ili pia uwawezeshe wanahisa wa KCB kununua hisa nyingi za benki hiyo.

Akifafanua Gupta alisema kuwa kwa sasa wateja, wadau na wanahisa wa benki hiyo watanunua hisa moja ya KCB Tanzania kwa bei 310/- kutoka 385/- bei iliyokuwa ikitumika katika kipindi cha wastani wa miezi sita iliyopita punguzo likiwa ni sawa na asilimia 21.

“Mpango huu unaotarajiwa kuanza rasmi Julai moja utakamilika Julai 23 mwaka huu na kwamba wanahisa waliofanikiwa kununua hisa za benki yetu kupitia kwa mawakala wetu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa punguzo la bei watatajwa Agosti 5 mwaka huu,” alisema Gupta.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa alisema hisa zitakazonunuliwa zitatumika katika nchi zote ambako benki hiyo inatoa huduma na zinauzwa kwa wananchi wote hata waso wateja wa benki hiyo.

Alisema pesa zitakazokusanywa zitatumika kupanua wigo wa utoaji huduma nchini na sio kwenye matawi ya nje ili kuongeza kiwango cha utoaji mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na uendelezaji wa makazi.

“Punguzo hili la bei litakaloanza Julai 1 mwaka Dar es Salaam huu litafanyika kwa wakati mmoja na Rwanda , Kenya na Uganda . Hivyo natoa rai kwa watu wote kuchangamkia mpango huu utakaowawezesha kuonesha ushindani wa kibiashara litakapoanza Soko la pamoja la Afrika Mashariki,” alisema Dk Mndolwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie alisema wamepanga kuifanya benki hiyo kuwa suluhisho la masuala ya kifedha kote inakotoa huduma zake.

Alisema kwa sasa benki hiyo imetoa fursa kwa wateja kupata huduma za kibenki bila shida yoyote. Huduma hizo ni zile zinazolenga aina zote za wateja wakiwemo wafanyabiashara, taasisi za serikali, mashirika mbalimbali, watu binafsi wakiwemo watoto.

Tofauti na hayo pia imeendeleza utamaduni wa kuwawekea akiba ya amana Watanzania kupitia mfumo wa benki ya Kiislam, benki kwa ajili ya wafanyabiashara, Ushirika pamoja na wateja wa kawaida. Pia kupitia huduma za Western Union , KCB pia inawawezesha wateja wake kutuma na kupokea fedha kwenye zaidi ya nchi 300 duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad