

Hatimaye Wizara ya Maliasili na Utalii imezipatia hadhi ya NYOTA hoteli za Tanzania ambapo 66 kati ya hotel 99 zilizokuwa kwenye kinyang’anyiro zimepata hadhi ya nyota kwenye ngazi mbalimbali.
Huku the Kilimanjaro Hotel Kempinski, Movenpick Royal Palm Hotel and Sea Cliff Hotel, wakiibuka na hadhi ya nyota 5 mahoteli mengine kumi yakiibuka na hadhi ya nyota nne (Four Star) nayo ni Golden Tulip Hotel, New Africa Hotel and Casino, Paradise City Hotel, Protea Hotel and Serviced Apartments, Southern Sun Dar es Salaam, Saadani Safari Lodge, White Sand Hotel, Giraffe Ocean View, Hotel Harbour View Apartments na Kinasi Mafia Hotel.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Mkurugenzi wa Giraffe Ocean View Hotel Dr. Charles Bekon amesema kuwa hayo ni mafanikio ya kujivunia kwani Hotel yao ina muda mfupi na hasa ukizingatia ushindani mkubwa wa biashara ambapo sekta ya Mahotel hasa ya kitalii imekamatwa na wageni.
Hata hivyo Dr. Bekon ametoa shukrani za dhati kwa watanzania wote wanaowaunga mkoni na kusisitiza kuwa pamoja na kupokea wageni wengi toka nje bado soko la ndani ni kubwa na linamchango wa kutosha.
Kwa upande wake Mheshimiwa Mwangunga alisema zilitumika 250milion shilingi za kitanzania kufanikisha zoezi hili huku wizara yake ikichangia Millioni 85 na Wizara ya biashara kupitia kitengo cha Tanzania Trade Integration Project wao wamechangia Million 176/-.
Kwa habari zaidi ya tukio hilo bofya
No comments:
Post a Comment