Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo,Silas Michael warembo hao watahudhuria mechi hiyo kwa ajili ya kuwashangilia ili kuwapa moyo Twiga Stars waweze kucheza kwa nguvu zote na hatimaye kuibuka na ushindi.
Alisema hudhurio hilo ni sehemu pia ya mikakati ya mlezi wa timu hiyo,Mama Rahma Al Kharoos ambaye amedhamini shindano hilo aliyepanga kuipeleka Twiga Stars nchini Marekani mwezi juni kwa ajili ya kujinoa zaidi.
Shindano la Miss Dar Intercollege linatarajiwa kjufanyika Mei 27 kwenye ukumbi wa Club Bilicanas ambapo warembo 15 watapanda jukwaani kuwania taji hilo wakisindikizwa na wasanii wa bongo fleva Amin na Barnabas.
Aidha kampuni za RBP Oil Industrial Technology Tz Limited, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Redd’s Orijino, Tanzania Daima, Vodacom Tanzania, Shear Illussion, Condy Bureau De Change, Ndege Insurance, Dotnata Decorations,Michuzi Blog,Mtaa Kwa Mtaa Blog,Full Shangwe Blog na Club Bilicanas wamejitokeza kudhamini shindano hilo.
No comments:
Post a Comment