


MAKULILO, Jr. Jumamosi Mei 22, 2010 amehitimu masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika Sanaa ya masuala ya Haki na Amani (Master of Arts in Peace and Justice) katika chuo Kikuu cha San Diego (USD) huko California.
Hii ni katika kuelekea katika Ph.D in Conflict Analysis and Resolution katika mwaka mpya wa masomo ujao.
Mdau MAKULILO, Jr. ana mpango wa kuja mapumziko nyumbani Tanzania akiambatana na mke wake. Katika mapumziko hayo atafanya semina na midahalo kwa watu kuhusu ni jinsi gani mtu unaweza kupata vyuo na ufadhili wa masomo (scholarships) ughaibuni.
MAKULILO, Jr. yeye mwenyewe amefaidika kwa kupata ufadhili wa masomo zaidi ya mara nne ndani ya miaka miwili na anapenda kuhakikisha wadau wengi wanafaidika na nafasi hizi zilizopo Ughaibuni.
Ratiba ya semina na mazungumzo maalum "special talks" itatangazwa baadaye mara baada ya maandalizi kuwa sawa.
KWA WANAOTAFUTA KOZI pamoja na UFADHILI WA MASOMO (SCHOLARSHIPS) UGHAIBUNI, usikose kutembelea:
SCHOLARSHIP FORUM http://www.scholarshipnetwork.ning.com/
MAKULILO BLOG http://www.makulilo.blogspot.com/
SCHOLARSHIP FORUM http://www.scholarshipnetwork.ning.com/
MAKULILO BLOG http://www.makulilo.blogspot.com/
MAKULILO, Jr.
San Diego, CA
No comments:
Post a Comment