
Ndugu Wanakijiji wa FotoBaraza,
Kwanza kabisa napenda kuwasalimu katika jina la ujenzi wa kijiji.Pili, napenda kuwashukuru kwa kuwa pamoja kwa takribani miaka miwili na vijimiezi.
Tatu, napenda kuwafahamisha kwamba ifikapo tarehe 1/6/2010, tutaufunga ukurasa huu wa fotobaraza.ning.com, kutokana na sababu zilizo nje kidogo ya uwezo wetu.
Lakini hata hivyo Waswahili hatuwezi kuondoka mtandaoni. Tayari tumeshahamia ploti mpya inayokwenda kwa jina la;http://www.fotobaraza.me/Utakapofika pale, kama wewe ni mwanakijiji hapa, hutakuwa na haja ya kujisajili, kwani uongozi wa kijiji umekwishakuhamishia ukurasa wako. Wewe ukifika tu pale anza kupandisha mapicha na kutupasha yanayojiri uliko.
Samahani kwa usumbufu wowote utakaokuwa umejitokeza, lakini hatua hii ni kwa ajili ya kutufanya tufurahie zaidi kijiji chetu.
Babukadja Sankofa
Mwenyekiti wa Kijiji
http://fotobaraza.ning.com
No comments:
Post a Comment