HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 23, 2010

Simulizi ya "Mfalme wa Ufisadi" - Sehemu ya Sita

"Ni kijana ambaye naye alikuwa kwenye kambi kama Tequila,...Sijui alitoroka au alikuwa na ruhusa ya kutoka, lakini masaa 24 baadae akawa amepata bastola na kuwacharaza risasi watu wawili" Rodney

Carter alikuwa akijihisi kuwa yu salama zaidi akiwa na Rodney. Hata hivyo saa tatu ya asubuhi bado ilikuwa ni mapema sana kwa watukutu wa mtaa wa Lamont kuwa wameamka na kuanza kuranda mitaani wakitishia maisha ya raia wema. Wafanyabiashara ndogondogo walikuwa tayari wameanza kupanga bidhaa zao kwa ajili ya mauzo na wenye maduka wakiwa mbioni kufungua maduka yao.

Rodney hakuwa mwanasheria kamili, kwani miaka kumi tangua aanze shahada yake ambayo ingemwezesha kuwa mwanasheria, bado hakuwa amefanikiwa kumaliza shahada ile. Mambo kadhaa yalikuwa yanamkwamisha. Akiwa na watoto wanne ambao wote walikuwa kwenye rika la balehe, na waliohitaji uangalizi wake wa hali na mali, fedha ya kulipia masomo yake na muda wa kuhudhuria darasani havikuwa upande wake. Hivyo kazi kubwa aliyokuwa akiifanya katika jengo la "The Cube" ilikuwa ni kuwasaidi wanasheria katika kesi zao, hasa katika suala la kwenda kukusanya vithibitisho vya ushahidi katika sehemu za matukio. Kwa maneno mengine unaweza kusema wakati wanasheria walifanyia kazi yao ofisini zaidi, Rodney alifanya kazi za uanasheri mitaani, hata hivyo kazi hiyo bado haikutosha kumfanya aitwe mpelelezi, labda mchunguzi.


Rodney ni kijana mweusi aliyetokea katika mitaa hii ya D.C. ambayo ilijaa umasikini na purukushani za kumtoa mtu uhai. Alizaliwa na kukulia kwenye mitaa hii, lakini yeye ni mmoja wa waliobahatika kuutoroka mtego wa madawa ya kulevya, na hatimae kujielimisha na kuweza kuishi maisha ya mtu aliyestaarabika. Alikuwa akisaidia wanasheria kadhaa walioajiriwa na serikali, japo wengi aliwatolea nje walipoomba msaada wake. Hakuwahi kumkatalia Carter hata mara moja, na kwa pamoja walikuwa wameshategua vitendawili vya kesi nyingi zilizokuwa zikisimamiwa na Carter.


Kwa pamoja, asubuhi ya leo wakajikuta wamesimama mahala ambapo Pumpkin alianguka na kupoteza uhai wake baada ya kushindiliwa risasi tano za utosi na Tequila. Kwa kiasi kikubwa ushahidi ulikuwa umeshapotea mahala hapa, hasa baada ya polisi kuwa wameshafika na kufanya uchunguzi wao mara kadhaa. Watu walioshuhudia tukio lile hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari kufungua mdomo wake na kuzungumza nao. Wale vijana wawili walioshuhudia kwa karibu Tequila akifyatua risasi walikuwa wamehama kabisa mtaa huu wa Lamont.


endelea kuupata uhongo huu kwa huku>>>>>

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad