HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 13, 2010

Wadau Kuweni Makini Na Vibaka Hawa

Habari Ndugu Othman,
kuna hili tukio la ukwapuaji wa kutumia gari ambao umekuwa ukishamiri sana hapa jijini kwa sasa,hivyo naomba uweke hapo mtaani kwetu ili wadau waweze kuwa makini na tukio kama hili.

Kuna tukio limetokea hapa Sinza maeneo ya Mapambano njia ya nyuma kama unaenda Mwenge kwenye miti mirefu bar moja inaitwa kwa jimmy .

Kuna vijana 2 walikuwa wanatembea njiani mmoja kabeba begi lake la vitabu ghafla gari ndogo ikampitia kwa pembeni mtu aliyekwepo ndani ya gari akakwapua begi la yule kijana ambapo kulikuwa na simu na karatasi zake .

Huyo kijana alipiga kelele kidogo nilikuwa mbele yao nikajua labda ni tatizo lengine kumbe wenyewe wameibiwa bei lao kwahiyo ile saloon car nyeupe ikakimbia moja kwa moja

Kijana aliyeibiwa anaitwa Erick Thomas Jongela simu yake anasema ilikuwa na line 2 moja ni 0715 241204 na 0756 816 770 hizi line zilikuwa kwenye simu hiyo iliyokwepo kwenye begi lililoibiwa

Mwenzake mwenye simu anaitwa Fadhili no yake ni 0713 76 59 05 Kwa mtindo huu jamani muwe makini mnavyotembea na mabegi yenu pamoja na mali zingine zisivutie sana wahalifu hawa .

Nimetoa kisa Hichi kama tukio la kweli lililomkuta mtu naamini tigo pamoja na voda kwa kushirikiana na vyombo vya dola vitaweza kufuatilia simu ya kijana huyo na kuweza kupata taarifa zingine zinazohusiana na simu hiyo toka ilipozimwa mara ya mwisho

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad