HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 15, 2010

URITHI WA VISASI!

Nadhani wote tunafahamu kwamba uhai wa binadamu ni kitu chenye thamani mno hapa duniani. Pia, tunafahamu kwamba uhai ndio chimbuko letu sisi wanadamu sambamba na viumbe vyote vilivyopo hapa duniani na sababu ikaitwa dunia.


Sasa basi , uhai wa binadamu ndio jambo ama suala pekee hadi wakati huu linalopatiwa ulinzi na jamii nzima.

Hivyo, binadamu yoyote yule anatarajia kuishi maisha uhuru yenye raha yenye uhakika kutokana na misingi ya kulindwa , kuheshimiwa na kupendwa na jamii hapa duniani.


Pindi linapotokea sakata ama sekeseke miongoni mwetu inatulazimu kutafuata suluhu kwa njia ya mazungumzo na si vinginevyo.


Pindi tunapofanya hivyo , tunakuwa tunafanya suala la kheri na ni njia salaama katika kujinasua na balaa .

Jamii ya Kitanzania imekuwa na historia na tabia ya kupendana , kulindana , kuheshimiana na kuvumiliana miongoni mwetu kwenye kuishi kwetu kila siku.


Hata hivyo , miaka ya karibuni kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nimekuwa nikisikia matukio ya kikatili hususani mkoani Mara.


Matukio hayo yanatia doa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kwa kuwa tumekuwa tunathaminiwa na kuheshimiwa mbele ya mataifa mengine huku tunatoa taswira mbaya kwa vizazi vyetu vya sasa na vijavyo kwa sababu matukio haya ni vigumu kutoka kichwani haraka .


Unakuwa ni urithi wa visasi kwa vizazi kwani tukio la kikatili la mwezi jana kama la kuua wanafamilia wanafamila tatu wa ukoo mmoja ni matokeo ya nini ?

Eti jamaa ambao wamefanya ukatili huo wamekusudia kulipa kisasi ! Kisasi kwa kuua wanafamilia tatu wa ukoo mmoja! Hii si mchezo.

Wamewachinja na kuwakata mapanga jamaa wa famila tatu wa ukoo mmoja huku wakiwemo watoto ambao hawafahamu kitu chochote kinachoendela !

Watoto ambao walikuwa tegemeo la baadaye la taifa hili na pengine labda kati yao walikuwemo ambao wangekuja kuwa viongozi mahiri ama wataalamu kwenye nchi hii.

Kwa kupitia makala hii fupi , urithi huu wa visasi unaotokea mara kwa mara huko mkoani Mara, usirejee tena kwani unaingiza dosari kwenye jamii yetu na taswira ya taifa hili, askari polisi ni lazima wafanye upelelezi haraka na kuwabaini watu ambao wamefanya ukatili huo kisha wafikishwe mahakamani .

Mimi kimasa kutoka www.kingkif.blogspot.com bado ninashauku kubwa kuona vitendo vya kikatili vya namna hii vinakomeshwa na huku nataka kufahamu kwa kina chimbuko la mauaji ya familia tatu wenye ukoo mmoja mkoani Mara.

Kwa mawasiliano nicheki :

kingkif07@gmail .com

ama simu

0714-077040 .

1 comment:

  1. Lakini naona hilo ni tatizo la watu wa mkoa huo tu kwa sababu mbona mikoa mingine hatusikii matukio ya kikatili ?

    ReplyDelete

Post Bottom Ad