HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 24, 2010

Kelele Za Mdau King Kif

Neno ama msamiati fadhila lina maana pana kama ukilingalia kwenye kamusi, lakini kwa jinsi linavyotumika kwa watu wengi kwa wakati huu na hasa linapokuja suala la rushwa ni kwamba inakuwa ni msaada,shukuran ama asante !

Hali hii ni kwa wahusika wote ambao wamehongana ama waliopeana hudumakwa kutoa ama kupokea rushwa.

Kwa wakati huu rushwa imetanda karibu kila sekita , iwe ni katika vyombo vya habari , hospitali , kwenye huduma za usafiri , bandarini , polisi, PCB, mamlaka ya leseni, ama sehemu yoyote ile.

Hivyo, neno fadhila linatamba kisawa sawa katika anga za rushwa!Ingawa watoaji na wapokeaji bado wana maneno yao mengine mengi ukiachilia mbali neno fadhila.

Tusibishane! Ni kweli rushwa inachukua nafasi kubwa kwa wakati huu katika maisha yetu ya kila siku Watanzania, na hii inatokana na kuwa Watanzania wengi hatuna ustarabu wa kusubiri , kwa mfano utakuta mtu anakwenda hospitali , huko akikuta kuna foleni ya kuingia kwa daktari
atataka kumhonga nesi eti amuingize haraka kwa daktari ili ahudumiwe yeye kwanza na kuwaacha wananchi wengine aliowakuta kwenye foleni!Kisa yeye anataka "favour ".

Huo ni upuuzi na bado kuna upuuzi mwingi kama huu karibu kwenye kila huduma hapa Bongo.Hebu siku moja jaribu ama jifanye unataka kukata tiketi ya ndege kwenda ulaya !Utajionea vioja na mambo mengi kwa hao maajenti wa hizo tiketi.

Lakini tutaendelea kuishi hivi hadi lini? Yaani mambo hayaende bila kutoa kitu kidogo? Hapana . Tutambue kwamba rushwa inadidimiza uchumi na maendelea kwa wakati mmoja.

Wananchi tukisema hapana kwa rushwa kweli itakuwa hapana . Tusiposema hapana kelele kama zangu za ukosefu wa maendeleo zitaendelea kupigwa na mimi na wengine leo , kesho hata siku nyingine.

Ni mimi Kimasa kutoka
www.kingkif.blospot.com
pia unaweza kunipata kwa
kingkif07@gmail.com
ama
0714-077040.

1 comment:

  1. Ni kweli kwamba sisi Watz maisha yetu tunayaendesha kwa rushwa kwa kiasi kikukbwa, lakini mdogo wangu king kif , sheria ya mwaka 1971 haikuanisha adhabu tofauti katika makosa ya rushwa!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad